May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kamati ya Bunge yapendekeza Jerry Silaa avuliwe ubunge wa PAP 

Jerry Silaa

Spread the love

 

KAMATI ya Haki,  Maadili na Madaraka ya Bunge, imemkuta na hatia Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa, katika tuhuma za kudharau mhimili huo na kupendekeza asimamishwe kuhudhuria mikutano miwili mfululizo, pamoja na kuondolewa uwakilishi wa Bunge katika Bunge la Afrika (PAP). Anatipoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mapendekezo hayo yametolewa leo Jumanne, tarehe 31 Agosti 2021, bungeni jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka, akiwasilisha taarifa ya uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili Silaa, za kudharau mhimili huo pamoja na kuuchonganisha kwa wananchi.

Akisoma taarifa hiyo, Mwakasaka amedai kwamba Silaa wakati anahojiwa hakuomba radhi wala hakujutia makosa aliyoyafanya kitendo kilichotafsiriwa kwamba ana mwenenso usiofaa na unaodhalilisha  hadhi ya nafasi ya mbunge kwa kusema uongo na kuwachonganisba wananchi na Bunge.

“Kwa kuwa Silaa mbele ya kamati hakukiri wala kujutia makosa yake, alionesha dharau na kudhaliliisha hadhi ya bunge,  kuchonganisha Bunge na wananchi. Hivyo kamati imemtia hatiani,” amesema Mwakasaka na kuongeza:

“Na kwa kuwa kanuni za kudumu za Bunge toleo 2020 inaipa Bunge mamlaka ya kupokea na kujadili mapendekezo ya kamati,  linaadhimia kuwa Jerry Silaa asimamishwe kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge mfululizo na aondolewe kwenye nafasi ya uwakiliwa wa Bunge PAP.”

error: Content is protected !!