Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kamati ya Bunge yamparura Simbachawene, Muhongo
Habari za SiasaTangulizi

Kamati ya Bunge yamparura Simbachawene, Muhongo

Prof. Sospeter Muhongo. Picha ndogo, George Simbachawene
Spread the love

KAMATI teule za Bunge za kuchunguza madini ya Almasi na Tanzanati leo zimewasilisha ripoti hiyo kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai huku baadhi ya vigogo wakiwa wamekalia kuti bovu, anaandika Dany Tibason.

Ripoti hizo mbili zilizowasilishwa leo bungeni ziliwataja vigogo wakiwemo, Mawaziri wa sasa, mawaziri wa zamani pamoja na mwanasheria wa serikali.

Wenyeviti wa kamati hizo waliwataja, baadhi ya vigogo akiwemo aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, aliyekuwa mwanasheria wa serikali Fredrick Werema, Waziri wa Tamisem, George Simbachawene, Prof. Sospeter Mhongo, Edwin Ngonyani pamoja na watendaji mbalimbali wa serikali.

Kwa nyakati tofauti kamati hizo zilisema kuwa kamati hizo zimebaini kuwepo kwa madudu mbalimbali huku viongozi katika nyadhifa mbalimbali kwa uchimbaji wa madini ya Tanzaniati pamoja na Almasi mbalimbali wakionyesha.

Kamati hizo za uchunguzi wa madini ya almasi na Tanzanite zimekuwa mwiba mkali kwa baadhi ya vigogo wa serikali pamoja na baadhi ya viongozi wakubwa ambao ni wastaafu.

Katika kamati ya Almasi iliyowasilishwa na Mussa Azzani Zungu hivyo taarifa ya Almasi, imesikitishwa na kampuni ya uchimbaji wa almasi kumzawadia kiongozi mkubwa ambaye alikuwa serikalini almasi yenye thamani ya dola milioni 20.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Musa Azan Zungu amesema wamebaini kuwepo kwa madudu mengi katika uchimbaji wa madini wa Almasi.

Amesema kuwa licha ya kuwa kuna madudu mengi, lakini bado maeneo mengi ya uchimbwaji wa madini ya Almasi hayajafanyiwa utafiti wowote.

Zungu amesema taratibu ya uchimbaji wa Almasi unafanywa kiholela huku akisema kuwa bado kampuni nyingi zimekuwa vinara wa kukwepa kulipa kodi au kubadilishana majina ya makapuni kwa madai ya kusingizia kupata hasara.

Akizungumzia kampuni ya uchimbaji wa madini ya Williamson, tangu mwaka 2007 hadi 2017 haijawahi kulipa kodi.

Amesema kuwa kampuni hiyo haikuweza kulipa kodi na Mrabaha kwa kisingizio kwamba inapata hasara, huku akihoji kama kweli kampuni inapata hasara kwa nini isifunge virago.

Hata hivyo, kamati imebaini kuwepo kwa taarifa tofauti kwamba taasisi za serikali ambazo zinahusika katika sekta ya madini.

Pia kamati imesema madini mengi ya Almasi yamekuwa yakiuzwa bila kulipia kodi hatua ambayo imeipotezea fedha ambazo zingetumika kuleta maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!