Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kamati ya Bunge yagomea ripoti, hekaheka Halmashauri Nyang’wale
Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yagomea ripoti, hekaheka Halmashauri Nyang’wale

Spread the love

HATUA ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), kugomea taarifa ya Halmashauri ya Nyang’wale, Geita kwa madai kwamba kuna ufisadi wa zaidi ya Sh 3 Bil, imetibua maofisa wake. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Kutokana na utata wa hesabu za halmashauri hiyo, LAAC imeiagiza Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalumu kwenye halmashauri hiyo ndani ya miezi mitatu ikiwa ni pamoja na kupitia miradi.

Maofisa katika halmashauri hiyo, wanatuhumiwa kutafuna fedha za umma kupitia miradi iliyobuniwa, huku wakishindwa kukabidhi baadhi ya vielelezo vya matumizi ya miradi.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 22 Agosti 2019, Abdallah Chikito, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema, taarifa ambayo ilitakiwa kuwasilishwa, imejaa ubadhilifu wa kutisha.

“Kwa sababu ya uzito ulipo kwenye taarifa hii, kwa mujibu wa kanuni zetu kifungu cha 15 na nyongeza 16, tumepewa jukumu la kusimamia fedha za umma katika Halmashauri za Mitaa.

“Lakini taarifa hii imejaa ubadhilifu, ndio maana Ofisi ya CAG ikatoa hati mbaya na tafsiri ya hati mbaya ni kwamba, Ofisi ya CAG wamekuta mapungufu mengi,” amesema na kuongeza;

“Kwa hiyo, kwa mamlaka tuliyopewa naagiza Ofisi ya CAG iende ikafanye ukaguzi maalum katika Halmashauri ya Nyang’wale, na tunafanya hivyo pamoja na kwamba kuna kesi ipo mahakamani,”amesema Chikota ambaye ni Mbunge wa Nanyamba (CCM).

Amesema, kuna upotevu wa fedha zaidi ya bilioni 3 na kuwa, kwenye ukaguzi, vitabu 50 vya kukusanyia mapato havikuwasilishwa.

“Lakini sio hivyo tu, kuna hati za malipo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.9, mpaka wanaondoka katika ukaguzi, vocha zenye thamani hiyo hazijaweza kuwasilishwa.

“Pia kuna uhamisho wa fedha bila kuonesha shughuli zinazoenda kufanya. Bilioni 1.7 zimelipwa kutoka akaunti moja kwenda nyingine na hakuna shughuli zilizofanyika, kuna malipo yasiyokuwa na viambatanisho yenye thamani ya shilingi milioni 339.7.”

Amesema, wakaguzi walioenda mwanzo, walikutana na changamoto ya miradi kuchelewa kukamilika ambapo alidai fedha shilingi milioni 400 ambazo zilikuwa zitumike kujenga kituo cha afya hazionekani zimeenda wapi.

Mwita Waitara, Naibu Waziri Ofisi Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), amesema ubadhilifu huo umeifedhehesha serikali.

“Tutawachukulia hatua kali na za kisheria waliohusika. Watapona kama watakuwa wamekufa tu, lakini kama wamestaafu lazima hatua za kisheria zichukuliwe.

“Haiwezekani milioni 500 zikapotea, hazijulikani zimeenda wapi, jambo hili limetufedhehesha. Pale kuna watoto wanakaa chini, kuna shida ya maji, haiwezekani,”amesema Jafo.

Denis Bandisa, Katibu Tawala za Halmashauri ya Nyang’wale amesema,  wamepokea maagizo hayo na watayafanyia kazi huku akidai, ukaguzi maalumu utawasaidia kujua ni nani walihusika na tuhuma hizo.

Aisack John, mwenyekiti wa halmashauri hiyo amesema, wataipokea kamati ya uchunguzi na watawasaidia katika kila kitachotakiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

error: Content is protected !!