December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kamati Miss Tanzania yajiondoa kuandaaji mashindano

Spread the love

KAMATI ya Miss Tanzania imekataa uteuzi wa kuandaa, kuendesha na kusimamia mashindano ya mrembo wa taifa. Anaandika Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Msemaji wa Kamati ya Miss Tanzania, Jokate Mwegelo amesema kamati yake imevunja ushirikiano na kampuni ya Lino International Agency kwa sababu ya kukosekana uhuru wa mipaka ya utendaji katika ushirikiano wao.

“Hapakuwa na mkataba mzuri unaoidhinisha mipaka ya kamati yetu na kufanya kazi hatua iliyosababisha kamati kushindwa kujua kama iliteuliwa kwa lengo la kutafuta fedha, kusimamia mashindano au kutoa ushauri,” amesema Jokate.

“Tumekuja kutoa taarifa ya kujitoa kwa kamati yetu kwenye mashindano ya Miss Tanzania yanayoandaliwa na Kampuni ya Lino International Agency. Awali Lino iliteuwa kamati yetu ili kusaidia kuandaa, kuendesha na kusimamia mashindano ya Miss Tanzania,” alisema Jokate.

Amefafanua kuwa Kamati yao ilipopewa jukumu la kuendesha mashindano ya Miss Tanzania ilipewa idhini ya kufanya kila kitu na Lino kuwa washauri, lakini hali halisi haikuwa hivyo.

“Lino ilitaka kuhodhi majukumu yote na kuiacha Kamati kuwa ya kutafuta wadhamini tu,” amesema.

Amesema Kamati yao ilifanya vikao vingi vya kuhakikisha mashindano yanaboreshwa na kubadilisha mfumo wa uendeshaji ili kuwa na muonekano mpya kama Lino ilivyoamua kuweka kamati mpya.

Kamati imewaomba radhi wadhamini ambao wameshafanya majadiliano nao kuhusu kutoa msaada wa kufanikisha mashindano yajayo.

Jokate amesema mawakala waliotuma maombi ya kutaka kuandaa mashindano kupitia kamati hiyo, sasa maombi hayo wayatume kwa kampuni ya Lino kwa kuwa wao hawatahusika tena na suala hilo.

error: Content is protected !!