July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kamati Kuu CCM kukutana

Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa CCM akizungumza na wajumbe wa chama hicho

Spread the love

 

KAMATI Kuu ya Chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), itakutana kesho Jumanne, tarehe 22 Juni 2021, jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Leo Jumatatu, kimefanyika kikao cha sekretarieti ya kamati kuu, kilichofanyikia makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma, ambacho kimeongoza na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.

Kikao cha kamati kuu, kitaongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema, maandalizi yote ya kikao hicho yamekamilika, “ni kikao cha kawaida cha kikatiba.”

error: Content is protected !!