August 12, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kamanda Sirro aonya wazazi, walezi

Spread the love

JESHI la Polisi limewataka wazazi na walezi kutoruhusu watoto wao kucheza kwenye madimbwi na maji yanayotembea katika kipindi hiki cha mvua za masiki zinazoendelea, anaandika Aisha Amran.

Rai hiyo imetolewa na Simon Sirro, Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam wakati kizungumza na waandishi wa habari leo.

Amesema kutokana na watoto wengi kupenda kucheza kwenye madimbi na maji yanayotembea bila ya kujua kina cha maji hayo, husababisha madhara mbalimbali ikiwemo magonjwa na kufa maji.

Pia ametoa tahadhari kwa wananchi wanaopenda kuvuka kwenye madaraja yaliyojaa maji kuwa makini na kasi ya maji ili kuepukana kifo.

Sambamba na hilo pia amewataka wachimba visima vya maji kuweka alama za maji ambazo zinaonekana ili kuepusha watu wenginne kutumbukia katika visima hivyo na hatimaye kuzama na kufa maji.

Aidha amesema watu wafukie mashimo ya takataka yaliyo pembezoni mwa nyumba zao ili kuepukana na mashimo hayo kujaa maji na kusababisha maafa makubwa.

error: Content is protected !!