Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Kamanda Shana afariki dunia
Habari Mchanganyiko

Kamanda Shana afariki dunia

Jonathan Shana (katikati) aliyekuwa Ofisa Mnadhimu wa Chuo cha Polisi Moshi (CCP),
Spread the love

ALIYEKUWA Ofisa Mnadhimu wa Chuo cha Polisi Moshi (CCP), Jonathan Shana amefariki dunia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Shana aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi mikoa mbalimbali ikiwemo Simiyu, Pwani, Mwanza na Arusha amefikwa na mauti usiku wa kuamkia leo Jumatano tarehe 16 Septemba 2020.

Msemaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha amethibitisha kutokea kwa kufo hicho cha Kamanda Shana akisema amefikwa na mauti baada ya kualazwa hospitalini hapo kwa siku 21 kati ya hizo tatu alikuwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi (ICU).

Enzi za uhai wake, Kamanda Shana alikuwa akionekana kujihusisha na shughuli za vyama vya siasa akiwa amevalia sare za polisi jambo ambalo lilikuwa likiibua mjadala.

 

Mrisho Gambo, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha wakati Shana akiwa kamanda wa polisi wa mkoa huo, ameandika katika ukurasa wake wa Instagram “nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Kamanda Shana.”

“Wiki iliyopita nilikwenda kumuona Muhimbili ambako alilazwa karibuni wiki tatu na nilipata matumaini makubwa. Jaman Kamanda Shana! Bwana ametoa na ametwaa – Jina la Bwana libarikiwe,” ameandika Gambo ambaye kwa sasa ni mgombea ubunge Arusha Mjini kupitia CCM

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

error: Content is protected !!