Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani
Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the love

KATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania na Marekani, Makamu wa Rais wa Taifa hilo kubwa duniani, Kamala Harris, amesema kuna “msururu wa hatua mpya” zilizoanzishwa kufikia azma hiyo. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … (endelea)

Kamala amezitaja hatua hizo leo Alhamisi tarehe 30 Machi 2023, wakati akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo yupo nchini humo kwa ziara rasmi akitikoea nchini Ghana ambako nako alifanya ziara.

Miongoni mwa hatua hizo ni kusainiwa kwa Hati makubaliano baina ya Tanzania na Benki ya EXIM ya Marekani ambayo itawezesha upatikanaji wa hadi Dola za Kimarekani milioni 500 kugharimia upelekaji wa huduma na bidhaa (export financing) Tanzania.

Amesema uwezeshaji huo utasaidia upelekaji wa bidhaa na huduma hizo katika sekta mbalimbali hususan, miundombinu, usafirishaji, teknolojia ya kidijitali na miradi ya nishati jadidifu.

Ametaja hatua nyingine kuwa ni kuzindua mradi wa ubia wa teknolojia ya 5G na usalama wa mtandao nchini Tanzania ambapo amesema hatua zinazochukuliwa za maendeleo ya teknolojia barani Afrika zitabadili kabisa dunia ijayo na zitanufaisha dunia.

Mbali na hayo amesema Marekani ipo mbioni kujenga kiwanda kikubwa barani Afrika kitakachozalisha malighafi zinazotokana na madini ya Nickel kwaajili ya kutengeneza betri za kuhifadhia nishati ya umeme.

Amesema kiwanda hicho kitachenjua madini ya nickel na madini mengine muhimu yanayochimbwa Tanzania, kikilenga kuzalisha nickel iliyotayari kutengenezea betri kwa ajili ya kupelekwa Marekani na soko la kimataifa ifikapo mwaka 2026.

Ameongeza kuwa kiwanda hicho kitazalisha malighafi hizo kwa kutumia teknoojia yenye kuzingatia usafi wa mazingira, walaalamu wa hali ya juu na hivyo kukuza sekta na ajira.

“Kuna fursa nyingi sana za kukua hapa kwahiyo utawala wetu unafanya kazi yakutambua fursa zingine za madini yatakayochakatwa kwenye kiwanda hichi kipya, ” amesema Kamala.

Kuhusu suala la usalama ameishukuru Tanzania kwa mchango wke katika kuimarisha amnai na usalama katika ukanda na kwamba watajadili kuhusu athari za vita ya Ukraine na Urusi na kuona namna ya kusaidia Tanzania katika kumudu mazingira ya sasa.

Pia amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa za kuwasaidia wanawake na kwamba amekuwa akisisitiza siku zote kuwa wanawake wanatakiwa kuweza kushiriki katika masuala ya jamii, siasa na uchumi, na kushiriki kwa usawa katika uongozi.

“Ukiinua uchumi wa mwanamke unainua uchumi wa familia na jamii na jamii yote itanufaika,” amesema.

Amesema jana alitangaza kutoa zaidi ya Dola bilioni moja kwa sekta zote binafsi zinazojipanga kusaidia kuwainua wanawake barani Afrika.

Pia amepongeza Tanzania kwa kuweza kudhibiti virusi vya Marburg na kushirkiana kwa uwazi na taasisi za kimataifa katika kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!