Thursday , 23 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kama mbunge anafungwa kimakosa, raia je?
Habari za SiasaTangulizi

Kama mbunge anafungwa kimakosa, raia je?

Mbunge Lijualikali (katikati) akiwa katika purukushani na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi.
Spread the love

KWA tukio la kufungwa na kushinda dhamana yake kwa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali na dereva wake Stephano Mgata unaweza kujiuliza ni wangapi wanafungwa magerezani bila hatia kwa sababu ya uonevu au upotevu wa sheria wa mahakimu wa mahakama za chini, anaandika Hamisi Mguta.

Weka pembeni ile dhana ya kwamba kutojua sheria si kigezo cha mtu kuwajibishwa na sasa fikiri kuhusu wanaojua sheria ambao ni mahakimu kuwawajibisha watu wasio na hatia.

Lijualikali alihukumiwa kifungo cha miezi sita, iliyotolewa Januari 11, 2017 na Mahakama ya wilaya ya Kilombero, Morogoro chini ya Hakimu Mkazi, Timothy Lyon kwa ‘kosa kufanya fujo na kusababisha taharuki’ lakini baada ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, kesi ikahamishiwa Mahakama Kuu.

Machi 30 Mahakama hiyo mbele ya Jaji Ama-Isaria Munisi ilimuachilia huru baada ya kupitia sababu za kupinga mbunge huyo kutiwa hatiani na kufungwa miezi sita jela.

Sababu zilizopelekea kuachiwa huru ni hati ya mashtaka kutofautiana na maelezo ya mashtaka yaliyotolewa dhidi yake, jambo ambalo linakiulizo je? hakimu aliyemuhukumu katika mahakama ya Kilombero hakuliona hilo.

Unaweza kusema kitu pekee kilichomsaidia Lijualikali kushinda kesi dhidi ya haki ni rufaa yake hivyo asingekata rufaa angeishia kumaliza miezi sita jela bila kuwa na hatia, lakini kuna wengi wanaohukumiwa kwa namna hiyo kisha wakashindwa kukata rufaa na kufungwa bila hatia.

Lijualikali na Mgata waliwakilishwa mahakamani na mawakili Tundu Lissu na Frederick Kihwelu huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na wakili wa serikali, Faraja Nchimbi.

Kwa mujibu wa Lijualikali mwenyewe baada ya kutoka gerezani amesema kitendo kilichofanyika kwa hakimu wa mahakama ya Kilombero kutoliona swala hilo kinamfanya aone kuwa amefanyiwa makusudi katika hukumu yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!