Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kali ya mwaka: JPM atumbua, ateua hapo hapo
Habari za SiasaTangulizi

Kali ya mwaka: JPM atumbua, ateua hapo hapo

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe (DAS ), Mtela Mwampamba
Spread the love

RAIS John Magufuli amemtumbua hadharani Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe (DAS ), Mtela Mwampamba na kumteua Mwanana Msumi kushika nafasi hiyo hapo hapo. Anaripoti Hamisi Mguta…(endelea).

Mwambapa ametumbuliwa leo tarehe 28 Juni 2020, wakati Rais Magufuli akizindua mradi wa maji wilayani humo katika Mkoa wa Pwani.

“….lakini pia hapa kuna tatizo moja, la mteule wangu mmoja DAS, nimeambiwa ana mambo ambayo hayaendani na maadili ya kazi yake, kwamba anachukua hata wake za watu. nilikwishamuonya siku za nyuma, nafikiri hakuweza kuonyeka.

“Na kwa sababu jukumu langu ni pamoja na kusimamia maadili nanidhamu za watendaji, ninakuagiza muheshimiwa Jafo (Suleiman Jafo – Waziri wa TAMISEMI) uongee na mheshimiwa Mkuchika (George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora) kwamba huyu kazi ya U-DAS nimeitengua leo,” amesema Rais Magufuli.

Pia Rais Magufuli ameagiza Mwampamba atafutiwe kazi ya chini inayoendana na uwezo wake, lakini pia kazi hiyo asifanye ndani ya Wilaya ya Kisarawe. Aliuliza kama ndani ya wilaya hiyo yupo anayefaa, na yafuatayo ndio mazungumzo yalivyokuwa:-

Rais John Magufuli

Rais Magufuli: Kwa hiyo utamueleza Mkuchika aniletee mapendekezo, au kama yupo hapa mnayemuona mwingine anayefaa faa U-DAS nimpe, kisha akamwita Mkuu wa Mkoa.

Rais Magufuli: Mkuu wa Mkoa… (Mhandisi Evarist Ndikilo).

Mkuu wa Mkoa: Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kuna Afisa Tawala, anaweza kabisa kufanya kazi hiyo.

Rais Magufuli: Ofisa Tawala yupo hapa? Njoo hapa ofisa tawala

Rais Magufuli: Ana elimu gani?

Aliyekuwa Afisa Tawala wilaya ya Kisarawe, Mwanana Msumi

Ofisa Tawala: Masters in Public Administration

Rais Magufuli: Una Masters ya Public Administration. Kuanzia leo wewe ni DAS, uendelee kufanya kazi, ili na nyinyi sana mkagombanie wanaume na Mkuu wa Wilaya (Jokate Mwegelo), halafu wote muondoke, ila hongera mama.

Rais Magufuli: Haya muandikieni barua leo aipate, huyu ndio DAS wa Kisarawe, sawa jamani? Mwanana Msumi oyeeee!

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!