Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Michezo ‘Kaka tuchati’ video kali, gharama haizidi elfu 60
Michezo

‘Kaka tuchati’ video kali, gharama haizidi elfu 60

Spread the love

KAKA tuchati. Linaweza lisiwe neno geni masikioni mwako hasa katika kipindi hiki kifupi ambapo wasanii wa muziki nchini Tanzania, Roma na Stamina wameachia ngoma yao waliyoipa jina hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tarehe 9 Mei, 2020 wasanii hao, Roma Mkatoliki and Stamina wanaounda kundi la ‘Rostam’ waliachia ngoma waliyoipa jina la ‘Kaka tuchati’ inayozungumzia hasa ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19).

Ngoma hiyo ambayo hadi leo Jumamosi tarehe 16 Mei, 2020 saa 5:20 asubuhi inashika namba moja ‘on trending’ katika mtandao wa ‘YouTube’ ikiwa imeangaliwa na watu 1,210,919.

Video ya wimbo huo yenye dakika 4:59 imekuwa gumzo na mjadala hasa ilivyofanywa na gharama zilizotumika kwani Roma ameifanya akiwa Marekani huku Stamina yeye akiwa Tanzania.

Hata hivyo, jana Ijumaa tarehe 15 Mei, 2020 katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV, Stamina na mwandaaji wa video hiyo ‘director’, Nicklass  walizungumzia maandalizi ya video hiyo na jinsi ilivyofanyika.

Wakijibu gharama zilizotumika kuandaa video hiyo, Nicklass alianza kwa kusema haikuwa kubwa kwani ni gharama za bando kupakua (download) video na picha zilizotumwa na Roma na zingine kutoka mtandaoni ambapo haikuvuka Sh. 60,000 kuikamilisha.

Akiwa bado hajamaliza, Stamina alisema jumla ya gharama zote kabisa zilizotumika hadi kukamilisha ni Sh 58,500, “sisi tunataka kufanya video itakayovunja rekodi kwa fedha kidogo.”

https://youtu.be/9EMWM_S1ioI

Akizungumzia jinsi video ilivyoandaliwa, Nicklass alisema aliwapa maelekezo kila mmoja, Stamina aliyekuwa Tanzania na Roma ambaye yuko Marekani kujirekodi katika simu kivyake kisha yeye akafanya kazi ya kuziunganisha.

“Tulitaka kitu halisi, hatukutana kutumia camera kurekodi kwani gharama ingekuwa kubwa sana,” alisema.

Alisema gharama zingine kati ya fedha hizo zilitumika katika kurekodi wanakwaya pamoja na mavazi waliyovaa.

Katika kipindi hicho, Juliana Shonza, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alipiga simu studio kuzungumzia suala jingine lakini mwisho alimweleza mtangazaji wa kipindi hiko akisema, “msalimie sana Stamina, mwambie ngoma nimeielewa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!