July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kaizer Chiefs dhidi ya Simba kupigwa Mei 15

Spread the love

 

MCHEZO war obo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kati ya Kaizer Chief dhidi ya Simba rasmi sasa utachezwa Tarehe 15 Mei, 2021jijini Johanesburg nchini Afrika Kusini. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Mchezo huo wa mzunguko wa kwanza utapigwa majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika Kusini na saa 1 usiku kwa saa za Tanzania.

Mara baada ya mchezo huo mechi ya marudiano itapigwa jijini Dar es Salaam siku saba baadae ambapo Simba atakuwa nyumbani kwenye dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 10 jioni.

Simba amefuzu hatua hiyo mara baada ya kumaliza kinara kwenye kundi A, akiwa na pointi 13 huku Kaizer Chief amemaliza katika nafasi ya pili kundi C akiwa na pointi 9.

Kama Simba atafanikiwa kufuka kwenye hatua hiyo na kutinga nusu fainali atakutana na mshindi wa mchezo kato ya Wydad Casablanca  na CR Belouizdad.

error: Content is protected !!