June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kairuki mgeni rasmi siku ya wajane Duniani

Mama mjane wa Makambako

Spread the love

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wajane Duniani. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Juni 23 mwaka huu ambapo kimkoa yatafanyika  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi leo Jijini Dar, Mwenyekiti wa Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA), Rose William Sarwatt amesema, siku hiyo itawakutanisha wajane wote nchini.

Sarwatt amesema, katika maadhimisho hayo pia wataweza kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili pamoja na utatuzi wake.

Maadimisho hayo ambayo yanafanyika Dunia nzima kwa hapa nchini yatabeba kauli mbiu isemayo, “Andika wosia kuepusha migogoro isiyokuwa na lazma”. Yataanzia stendi ya stesheni hadi sehemu husika.

“Kauli mbiu hiyo imekubalika na takrbani ya wajane wote nchini, kutokana na changamoto zetu kufanana, ikiwemo ya kushuka kwa uchumi ndani ya familia pindi mume anapofariki,” amesema Sarwatt.  

Aidha amesema, changamoto kubwa wanayoipigia kelele wajane wengi nchini ni uchumi kuporomoka pindi wakiondokewa na wenza wao, hivyo tatizo hilo pia huongeza   idadi ya watoto yatima mitaani.

Mbali na kupata changamoto hizo Sarwatt amesema, uwepo wa TAWIA umekuwa msaada mkubwa na kimbilio la wajane wengi kwani kimekuwa msari wa mbele kuwasaidia.

Licha ya wajane wengi kuonekana kukata tamaa ya maisha, TAWIA ilianzisha miradi mbalimbali ya kuweza kuinuana kimaisha ikiwemo ya kufanya biashara ndogondogo.

Na kwamba biashara hizo na michango mbalimbali imewasaidia kuwapeleka watoto shule pamoja na kujikimu katika maisha yao.

“Nichukue fursa hii kuwakumbusha wadau mbalimbali ambao wanaweza kutusaidia, ili tuweze kuwafikia wajane wengine waliopo vijijini ambao hatuwezi kuwafikia. Pia tunaomba serikali itusaidie kupata takwimu ya wajane  wote nchini, ili iwe rahisi kuwafikia,” amesema.

error: Content is protected !!