July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kairuki awapa matumaini wanawake

Spread the love

ANGELA Kairuki, Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amewahakikishia wanawake hadi kufikia mwaka 2030, watakuwa wamefikia usawa wa kijinsia wa hamsini kwa hamsini, anaandika Happyness Lidwino.

Kairuki amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanawake waliohudhulia kwenye mjadala ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia (TGNP) kujadili usawa wa hamsini kwa hamsini.

Wakati akihutubia katika mjadala huo ambao pia ulihudhuliwa na wanaharakati mbalimbali akiwemo Jenelali Ulimwengu ambaye ni Mwanasheria na Mwanahabari; Ruth Meena, mbobezi wa masuala ya jinsia na uongozi Kairuki amesema, serikali ipo kwenye utekelezaji wa mikakati ya kumkomboa mwanamke.

Amesema, Tanzania ni moja ya nchi kati ya zinazoheshimu na kuthamini haki za wanawake na kwamba imesaini mikataba mingi ya ukombozi wa mwanamke ni lazima itatekeleza.

Waziri Kairuki ameongeza kuwa, nchi itakapofika kwenye uboreshaji wa Kura ya Maoni ya Katiba Mpya wanawake wasimame kutetea hamsini kwa hamsini ili iweze kupatikana na wanawake wapate ukombozi.

“Kama ilivyokuwa kwenye kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani inayotarajiwa kufanyika kesho tarehe 8 Machi kwamba, hamsini kwa hamsini ifikapo mwaka 2030 inawezekana tuongeze juhudi.

“Mimi pia nitajitaidi kuungana na wanawake wenzangu katika kutimiza hilo na tutafanikisha” amesema Kairuki

Pia amesema, serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo ya kuziondoa sheria kandamizi, kukomesha masuala ya ukeketaji pamoja na haki za mwanamke ikiwa ni pamoja kumiliki aridhi sawa na mwanaume.

“Mwanamke anayohaki sawa na mwanaume.Hakuna mwanamke dhaifu kila mwanamke akiwezeshwa anaweza kama ilivyokuwa viongozi wa kike waliopo madarakani wanafanya kazi vizuri”

Amesema, kama serikali imejipanga kumpa mwanamke na mtoto wa kike vipaombele ili kumwezesha kufikia ndoto zake ikiwa ni pamoja na kuongeza shule za wasichana, kuboresha miundombinu na kuwawezesha wanawake kiuchumi.

“Naupongeza mtandao wa TGNP na asasi nyingine zinazomtetea mwanamke kwa juhudi zao katika kuwasaidia wanawake na watoto katika kutoa elimu kwa wanawake na kuwafanya wajiamini na kujikomboa nawaahidi tupo pamoja” amesema Kauruki

Naye Ulimwengu wakati akichangia mjadala huo ametoa rai kwa serikali na wanaharakati mbalimbali nchini kuanza kutoa elimu juu ya masuala ya kijinsia mapema kuanzia katika shule ya msingi hadi vyuoni.

“Kunabaadhi ya wanawake hawatambui wajibu wao na haki zao hivyo wanachangia katika kumkandamiza mwanamke mwenzie na kujiona wao ni watumwa siku zote. Hususani vijijini wanahitaji elimu zaidi ili wajitambue kwamba wanahaki kama wanaume”.amesema Ulimwengu.

error: Content is protected !!