May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kahata aondoka rasmi Simba

Spread the love

 

KIUNGO Raia wa Kenya Francis Kahata ameachana rasmi na klabu ya Simba mara baada ya mkataba wake kumalizika na kuwashukuru viongozi pamoja na benchi la ufundi katika kipindi chote alichokuwepo ndani ya klabu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kahata anaondoka ndani ya klabu ya Simba mara baada ya kuitiumikia katika misimu miwili toka alipojiunga nayo Tarehe 4, 2019 akitokea klabu ya Gori Mahia ya nchini Kenya.

Kupitia ukurasa wake wa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram Kahata aliandika maeno ya kuwaaga mashabiki na wanachama wa klabu hiyo mara baada ya kufikia makubaliano na uongozi huo juu ya kuondoka kwake.

“Ilikuwa safari tamu, yenye kumbukumbu na machungu tangu siku niliyotua nchini Tanzania. Nilipewa support na upendo kutoka kwa timu ya uongozi chini ya Mo Dewji, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki wa Simba.” Aliandika kiungo huyo

“Shukrani zangu zinakwenda kwa kocha mkuu Didier Gomes kwa nafasi aliyonipa kuiwakilisha jezi nyekundu, wachezaji wenzangu kwa ushirikiano walionipa na wote tuliokuwa pamoja katika safari hii.”

Aidha mchezaji huyoa liongezea kuwa anaondoka ndani ya klabu hiyo huku akijivunia mafanikio aliyoyapata ikiwemo kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Ninaondoka nikiwa kifua mbele huku najivunia mafanikio ndani ya klabu. Umefika wakati wa kusema kwaheri kwenu nyote. Natakiwa kutafuta changamoto mpya na nafasi sehemu nyingine.

Daima nitaishukuru Simba kwa kila kitu na kumtakia kila la heri kila mmoja kwenye mechi zijazo na misimu pia. Miaka miwili ilikuwa yenye faida.” Aliandika mchezaji huyo

error: Content is protected !!