Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Michezo Kagere, Wawa, Banda wavunjiwa mikataba Simba
MichezoTangulizi

Kagere, Wawa, Banda wavunjiwa mikataba Simba

Meddie Kagere
Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba imevunja mikataba ya nyota wake wanne wa kigeni wakiwemo mastaa wao aliokuwa tegemeo katika kikosi hicho kwa misimu kadhaa, beki wake Raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa na mshambuliaji wake, Mnyarwanda, Meddie Kagere. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Mbali na mastaa hao wawili tegemeo, nyota wengine wa kimataifa waliotemwa ni Peter Banda aliyesajiliwa kwenye dirisha kubwa la usajili mwezi Agosti na kiungo mshambuliaji Dancan Nyoni Raia wa Malawi ambaye ameshindwa kuonesha makali yake toka asajiliwe klabuni hapo.

Simba imeamua kuvunja mkataba na wachezaji hao, ili kupata nafasi ya kusajili wachezaji wengine wa kigeni kwenye dirisha dogo la usajili.

Pascal Wawa

Ikumbukwe hivi karibuni klabu hiyo ilivunja mkataba kwa makubaliano maalumu na kocha wake msaidizi Thiery Hitimana raia wa Burundi.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameamua kufanya maboresho kwenye kikosi chao kufuatia kusuasua hivi karibu.

6 Comments

 • Matatizo yenu na Yanga ni haya hapa:
  1) Wachezaji wanachaguliwa na viongozi.
  2) Hamna ubunifu wa kuwKuuza Simba/Yanga B na Simba/Yanga watoto.
  3) Mnachukuwa wachezaji wazee (27+) na mnashindwa kujua time huhitaji miaka mitatu kujengwa. Sasa hao wageni watajengaje timu?
  4) Hamjawahi kuchukua kocha msomi kama marehemu Syler Said Mziray. Wapo tele wazawa waliosomea michezo Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam. Nyie mnataka wazungu tu kubabaisha wachezaji.
  5) Mliwanyang’anya wanachama haki yao kwa kuuza 61% ya klabu. Hakuna kitu kama hicho duniani.
  6) Klabu za wanachama wanamfukuza mwekezaji. Simba mmeliwa kwenu. Yanga mpo njiani. Niombe Mo na Manji waondoke na kuanzisha time zao. Mwekezaji wa Manchester United yuko hatihati sasa klabu ikiendelea kusuasua.
  7) Ningefurahi kama tunazo Mo Sports Club, Manji FC na Azam FC kama klabu za binafsi ligi kuu. Ligi zote kuu za Ulaya na Amerika ya Kusini ziko hivyo.

 • Kwa Banda big mistake! Kwa Kagere angeachwa amalize mkataba. Kwan ndio goal getter . Wawa walichelewa alitakiwa aachwe dirisha kubwa.

 • Hv hawa viongozi wanashauriana na nani?huyu kijana Banda huwezi kumjudge mapema hivyo alitakiwa aachwe azoee mazingira ukizingatia na umri wake,tatizo la vilabu vyetu hivi vinazingatia zaidi mafanikio ya usiku mmoja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

error: Content is protected !!