Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari Kagere , Lwanga waagwa kwa Furaha
HabariMichezo

Kagere , Lwanga waagwa kwa Furaha

Spread the love

 

Walio kuwa wachezaji wa klabu ya Simba Meddie Kagere pamoja na Thadeo Lwanga wameagwa rasmi leo Agosti 6 2022 katika kilele cha maadhimisho ya Simba day yaliyo fanyika katika uwanja wa Benjamin
Mkapa. Anaripoti Damas Ndelema….(Endelea)

Tamasha hilo la kiburudani ambalo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kutambulisha wachezaji pamoja na benchi la ufundi litakalo itumikia klabu hiyo pia kutoa fursa kwa mashabiki kuweza kuiona timu yao kabla ya msimu kuanza

Akizungumza katika tamasha hilo lilohudhuriwa na mamia ya wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo mshambuliaji raia wa Rwanda Meddie kagere aliwashukuru mashabiki kwa upendo wao kipindi chote alicho kuwa Simba na anajivunia kuwa mmoja ya wachezaji walio changia mafanikio ya Simba kwa kipindi hichi cha miaka mitano na pia anawatakia mafanikio mema katika msimu mpya unaoanza hivi karibuni

“Asante kwa mapenzi yenu na ushirikiano wenu katika kipindi chote nlichokua Simba nanyi pia niwatakie mafanikio mema na bora katika msimu unaokuja “Alisema mshambuliaji huyo

Aidha pia mchezaji Thadeo lwanga nae aliwashukuru mashabiki kwa mapenzi yao na kuwaombea wawe na Mafanikio mema pia aliwashukuru viongozi na wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliompatia kipindi chote walichokuwa wote Simba

“Napenda kumshukuru Rais wa heshima wa klabu mwenyewe kiti pamoja na viongozi bila kusahau wachezaji wenzangu pamoja na mashabiki wote Asanteni kwa upendo na ushirikiano “

Wachezaji hao waliofanikiwa kutwa mataji na wakiwa na klabu hiyo watakumbukwa kwa mchango wao hilo lilithibitishwa na mashabiki pale walipokuwa wakipita uwanjani kuwaaga na mashabiki kuwapokea kwa furaha na shangwe kubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!