Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kagame agomea nchi yake kupokea tena wakimbizi wa DR Congo
Kimataifa

Kagame agomea nchi yake kupokea tena wakimbizi wa DR Congo

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Spread the love

 

RAIS wa Rwanda Paul Kagame anasema nchi yake haitatoa tena hifadhi kwa watu wanaokimbia migogoro katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mashirika ya kimataifa yameripoti … (endelea).

Miongo kadhaa ya ukosefu wa utulivu mashariki mwa DRC imelazimisha wakimbizi wengi kuvuka mpaka na kuingia Rwanda.

“Hili si tatizo la Rwanda,” BBC Swahili imemnukuu Kagame na kuongeza: “Ninakataa kwamba Rwanda inapaswa kubeba mzigo huu. Dunia nzima imeshindwa kuelewa tatizo na kuingia mashariki mwa DR Congo,” alisema Kagame.

Tishio halisi kwa usalama – kwa maoni yake – ni kile anachoelezea kama mabaki ya vikosi vya Wahutu wenye itikadi kali ambao walijaribu kuliangamiza kabila lake la Kitutsi katika mauaji ya kimbari ya 1994.

Rwanda inashutumiwa kwa kuunga mkono kundi la waasi la M23 – jambo ambalo nchi hiyo imekuwa ikikanusha.

Kundi hilo la waasi limeteka maeneo mengi katika miezi ya hivi karibuni, na kutuma makumi ya maelfu ya wakimbizi kuvuka mpaka na kuingia Rwanda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!