MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema jumla ya mifugo 1,257 imekufa mkoani humo kwa kukosa maji na malisho kutokana na ukame uliokumba mkoa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).
Kagaigai ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Januari, 2022 wakati akitoa taarifa ya Mkoa huo kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekwenda kuzindua Tamasha la Utamaduni mkoani humo.
Kagaigai ameitaja mifugo hiyo iliyokufa kuwa ni ng’ombe 841, kondoo 406 na punda 10
Amesema licha ya mafanikio na kazi mbalimbali za maendeleo zinazoendelea, mkoa huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutonyesha kwa mvua za vuli, hali ambayo imesababisha ukame na vifo vya mifugo.
“Uongozi wa mkoa unaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na hali hiyo. Pamoja na vifo hivyo vya mifugo, hali ya chakula bado ni nzuri, na Mkoa unachakula cha kutosha.
“Pamoja na ukame huo mkoa umejitosheleza kwa chakula hii ni kutokana na kuwa na ziada ya uzalishaji wa chakula tani 40,790 za wanga na tani 10,147 za mikunde zilizopatikana katika msimu nwa mvua 2020/2021.
Leave a comment