January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kafulila: Nilijua Ikulu itamsafisha Maswi

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila

Spread the love

MBUNGE wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila amesema kitendo cha Ikulu kumsafisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi, alikitarajia. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Wiki iliyopita Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni alisema uchunguzi uliofanywa dhidi Maswi, haukumkuta na hatia yeyote katika kashfa ya ukwapuaji fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Kafulila amesema “Uamuzi wa Ikulu kumsafisha Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo na Maswi nilitarajia kwa sababu nina ushahidi wa barua ambao unaonesha Ikulu kuhusika katika sakata hili”.

“Ombeni Sefue anahusika na yeye huyo huyo ndio achukue hatua ulitegemea nini? Binafsi nimetimiza wajibu wangu,” amesema Kafulila.

Kafulila amesema, kufuatia Ikulu kumsafisha Maswi, anatarajia kuwasilisha hoja kwa viongozi wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kisha wataamua hatua za kuchukua.

“Naamini “Escrow Scandal” (Kashfa ya Escrow) itakiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM) madarakani kama “Goldenberg Scandal” Kashfa ya Goldenberg ilivyokiondoa chama cha Kenya African National Union (KANU) madarakani na mhusika akiwa huyu huyu Sethi,” Kafulila amesema.

Umamuzi wa kumrejesha Maswi kazini au kumpangia majukumu mengine unakuja siku 10 baada ya Kafulila kutunukiwa tuzo na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRD) kwa kuibua na kusimamia Kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow Bungeni.

error: Content is protected !!