July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kafulila aufukuzia Ubunge Kigoma

Spread the love

MBUNGE wa zamani wa jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila amevuka kikwazo muhimu cha kesi aliyoifungua kupigania kiti chake cha ubunge baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kuipangia siku ya kusikilizwa. Anaandika Jabir Idrissa … (endelea).

Jaji Sam Rumanyika amesema kwamba mapingamizi yaliyowekwa na mawakili wa serikali kutaka kesi hiyo ifutwe kwa madai kuwa haina msingi yametupiliwa mbali.

Moja ya maamuzi muhimu yaliyofanyika leo mjini Tabora, baada ya Jaji Rumanyika kusikiliza mapingamizi ya upande wa walalamikiwa tangu Januari 11, ni kuwa mahakama inayo mamlaka ya kusikiliza na kuamua ombi la mlalamikaji ambaye ni Kafulila, kutaka mahakama imtangaze yeye ndiye mshindi wa uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

Na kwa sababu hiyo basi, Jaji Rumanyika ameipangia kesi hiyo Na. 2/2015, kusikilizwa tarehe 28 Januari.

Mawakili wanaomtetea Husna Mwilima aliyetangazwa mshindi wa ubunge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi, waliwasilisha mapingamizi matatu wakijenga hoja ya kutaka mahakama iitupe kesi hiyo.

Madai au mapingamizi yaliyowasilishwa na mawakili hao ni:

  • Hati ya mashitaka haina vifungu vya sheria vinavyoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
  • Ombi la mlalamikaji (Kafulila) kutaka atangazwe mshindi halimo ndani ya uwezo wa mahakama kwa kuwa mamlaka hayo ni ya Tume ya Uchaguzi, na
  • Ombi la kwamba mahakama ipitie fomu za matokeo halitambuliki kisheria.

Mahakama imeamua kwamba:

  • Hoja kwamba hati ya mashtaka haina au haijaweka sheria inayoipa mamlaka mahakama kusikiliza na kuamua kesi hii haina msingi kwa kuwa kesi ya uchaguzi sio sawa na maombi ya kawaida, na zaidi Sheria ya Uchaguzi ya 2015, kifungu 110 kimesisitiza wazi kuwa mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za uchaguzi na hivyo haikuwa na ulazimia kutaja ukweli ulio bayana.
  • Hoja kwamba mahakama haina uwezo wa kutangaza mshindi haina msingi kwa sababu Sheria ya Uchaguzi ya 2015, Kif. 112 kimeweka wazi mamlaka ya mahakama kuwa ni pamoja na kutangaza mshindi aliyechaguliwa na hivyo Kafulila ana haki ya kuomba ombi hilo.
  • Kuhusu pingamizi kuwa ombo la Kafulika la kuomba kupitiwa kwa fomu 21B za kila kituo, Mahakama imeelekeza kuwa dhana ya ombi hilo inamezwa na ombi la mlalamikiaji kutangazwa mshindi hivyo halina sababu kuwepo.

Kwa mujibu wa malalamiko ya Kafulila, alipata kura nyingi katika uchaguzi uliofanyika kwa utulivu, na kazi ya kuhesabu kura na kujumlisha, ilikwenda vizuri lakini yalipokuja kutangazwa matokeo, alitangazwa kuwa ameshinda.

Kafulila amekuwa akihangaikia kesi hiyo ifanikiwe, akidai kuwa aliporwa haki yake ya ushindi ambayo badala yake Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Kigoma Kusini alimtangaza Mwilima kuwa ndiye mshindi.

Kafulila aligombea ubunge kutetea kiti hicho cha Kigoma Kusini kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, akiungwa mkono na vyama vya Chadema, CUF na NLD ambavyo kwa pamoja viliunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

error: Content is protected !!