Sunday , 25 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kafulila asimulia machungu aliyokutana nayo kwa Escrow
Habari za SiasaTangulizi

Kafulila asimulia machungu aliyokutana nayo kwa Escrow

Spread the love

ALIYEKUWA mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila ameibuka na kusimulia kuwa sakata la Escrow ni miongoni mwa mambo yaliyosababisha akapata ugumu katika mambo mengi na kwamba kwa sasa amepumua baada ya kuonekana kuna watu wapo nyuma yake wanamuunga mkono, anaandika Mwandishi Wetu.

Akizungumza na Mwanahalisi Online, Kafulila alisema mtu asisite kuanzisha jambo lolote kwa kuhofia kupitia magumu, kwa kuwa unakuwa unasimamia ukweli na ule ukweli huo utakuja kusimama hata kama umekufa.

“Niliibua jambo hili bungeni, likasababisha ugumu katika mambo yangu mengi, anapotokea mtu akaona mchango wako sio jambo la kawaida, katika masuala haya ya ufisadi mtu asihofu wala asisite kuanzisha jambo lolote kwa kuhofia kupitia magumu, kwasababu unakuwa umesimamia ukweli ule ukweli utakuja kusimama hata kama umekufa, ukweli haufi, utasimama wenyewe milele,” amesema.

Kutokana na ujasiri wake kwa kuibua jambo hilo la Escrow, Kafulila amealikwa nchini Marekani kushiriki  programu ya masuala ya ufisadi kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa bungeni ya kupambana na ufisadi.

Kafulila ameyasema hayo akizungumza na MwanaHALISI Online ikiwa ni siku chache baada ya rais Magufuli kumsifu kwa kuibua sakata la Escrow.

Amesema mapambanao ya ufisadi lazima yawe endelevu na kwamba kuna haja ya kuangalia sheria ili kuziimarisha kwa ajili ya kuhakikisha mapambano ya rushwa yanaimarishwa.

“Kwa miaka mingi suala hili limetafuna uchumi na ndiyo chanzo cha umaskini kwenye taifa letu, linapaswa kuangaliwa kikatiba ili kuhakikisha ufanisi wa ofisi za Mdhibiti na Mkaguzi waHesabu za Serikali (CAG), DPP na Takukuru,” amesema.

Aidha, Kafulila amesema Marekani imempa nafasi hiyo kama tuzo ya heshima baada ya kufichua mafisadi waliofanya wizi wa fedha za umma.

Ikumbukwe kuwa watetezi wa haki za binadamu nchini walimpatia tuzo ya heshima iliyotambulika kama ‘Mpiga Filimbi’ kutokana na sakata hilo kabla ya Marekani kumtambua na kumpa heshima hii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

Habari za Siasa

Mbarala ajitosa kumrithi Zitto, aahidi kuipa ushindi ACT-Wazalendo uchaguzi mkuu

Spread the loveKATIBU wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalum...

error: Content is protected !!