January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kafulila ajigamba mafanikio jimboni

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila

Spread the love

WAKATI wabunge 51 wakiangushwa katika mchakato wa kura ya maoni, ambao unatumika kumpata mgombea atakaye kiwakilisha chama katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, David Kafulila – Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR – Mageuzi) amepita bila kupigwa ndani ya chama chake. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Sababu kubwa inayotajwa na wananchi kusababisha wabunge hao kuangushwa ni; kushidwa kuwawakisha wananchi Bungeni na kushidwa kushirikiana na wananchi wanaowaongoza katika kutatua kero zinazowakabili.

Kwa upande wa Kafulila, hali ni tofauti. Anajivunia kuwajibika ipasavyo. Japo hakufikia malengo kwa asilimia 100, lakini kwa hatua iliyofikia katika kutatua changamoto za wananchi wake katika jimbo analoliongoza na ngazi ya taifa anajihakikishia kurudi bungeni iwapo tu “matokeo ya uchaguzi hayatachakachuliwa.”

Katika mahojiano na MwanaHALISI Online Kafulila anasema, “sikuahidi kutatua kila kero na matatizo ya jimbo. Lakini niliahidi kuonesha tofauti ya jimbo kabla na baada ya miaka mitano ya uongozi wangu.”

“Niliahidi kujenga heshima ya jimbo letu bungeni na taifa kwa ujumala kupitia hoja niliyoitoa ya ESCROW. Serikali ilivunjika. Kuivunja serikali ndio kilele cha uwajibika katika vita dhidi ya mafisadi,” anasema Kafulila.

Akizungumzia kuhusu mabadiliko ya jimbo hilo Kafulila anasema alipewa jimbo ikiwa ukanda mzima wa ziwa hauna huduma ya simu, leo kata zote za ukanda huo zina huduma hiyo.

“Nimepewa jimbo ukanda wa ziwa haupitiki kwa barabara; Leo barabra zimebaki kilomita chache ifike Kalya na madaraja zaidi ya 19 madogo yamejegwa. Kata ya mtego imeunganishwa kwa barabara,” anasema Kafulila.

Amehakikisha serikali inatekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara mbili za lami zenye urefu wa Kilomita 126 na kufanya jimbo hilo kuwa na mtandao mrefu wa lami kuliko jimbo lolote mkoa wa Kigoma na ndio jimbo pekee lililopata lami 2010- 2015 katika mkoa huo.

Mbali na kero ya barabara, jimbo hilo halikuwa na vivuko bora hasa ubovu wa kivuko cha Ilagala. Kwa sasa kuna kivuko bora kutoka Uholanzi chenye thamani ya Sh. 3 bilioni ingawa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ujenzi wa kivuko hicho haukuwemo.

“Nimehakikisha serikali inatekeleza ahadi ya ujenzi wa daraja malagarasi iloshidwa tangu mwaka 1979 kwenye mpango wa kwanza wa maendeleo na hata miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Rais Kikwete,” amesema Kafulila.

Pia, jimbo hilo halikuwa na utaratibu wa kusomesha watoto yatima au wale wanaotoka katika familia zisizojiweza. Kafulila amefanikiwa kusomesha watoto 200 huku wengine wakifanikiwa kumaliza na kuendelea na elimu ya juu.

Katika kuhakikisha maendeleo katika sekta ya elimu yanapanuka katika jimbo analoliongoza Kafulila anasema, “Nimepeleka vifaa maabara (mobile laboratory) katika shule za sekondari 17, rekodi ambayo hakuna jimbo katika mkoa wa Kigoma limefikia hatua hiyo.”

“Nimepeleka vifaa vya computers, printers, fax na mashine za photocopy katika shule za sekondari tano za; Ruchungi, Nguruka, Kalenge, Sunuka na Ilagala na kutumia mfuko wa jimbo kuanzisha ujenzi wa shule ya sekondari Basanza,” ameeleza Kafulila.

Aidha, katika kukabiliana na changamoto ya afya hasa afya ya mama na mtoto, amefanikisha ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Kalya kwa hoja na mchango wa moja kwa moja;

Amefuta tatizo la vitanda na magodoro katika kituo kikubwa cha afya Nguruka kwa kupeleka magodoro 20, vitanda 20, shuka 30 na kuchangia juhudi za ujenzi wa kituo cha afya Kazuramimba.

Kuhusu kupunguza kero ya upatikanaji wa maji safi na salama, Kafulila amehakikisha jimbo hilo linapata miradi mitano mikubwa ya maji Rukoma, Nguruka, Uvinza, Kandaga na Ilagala. Amesaidia upatikanaji wa visima vifupi kata ya Mtego, Chagu na anaendelea na juhudi hizo katika kata ya Mgaza.

“Nimehakikisha serikali imekubali kulipa mafao ya waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa chumvi Uvinza tangu mwaka 1999. Niliahidi kuhakikisha kiwanda cha chumvi kinaacha kutumia kuni kutokana na uharibifu wa mazingira. Serikali ipo tayari kukifunga mpaka hapo mwekezaji atakapobadilisha teknolojia,”amesema Kafulila.

Mafanikio mengine ambayo Kafulila anajivunia kupatikana wakati wa uongozi wake katika jimbo hilo ni ujenzi wa mtandao wa umeme ambapo kwa kuanzia unajegwa Ilagala, Mwakizega, Simbo, Kandaga, Kazuramimba, Uvinza na Basanza. Pia anaendelea kupigania tarafa ya Nguruka ipate kituo cha umeme. Ukanda wa ziwa utapata umeme baada ya mpango wa REA unaofuata.

Kuhusu kuwainua wajasirimali wadogo anasema aliishawishi benki ya Twiga na kupeleka jimboni kwake mafunzo ya banki vijijini (Vikoba) na kufanikisha Halmashauri ya jimbo hilo kupata trekta 10 za mkopo kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Ametoa vifaa vya michezo kama jezi na mipira kwa timu za vijiji vyote jimbo zima. Na baadhi ya kata zimeshiriki katika michezo kiwango cha ligi.

Katika kuimarisha utwala bora jimboni kwake Kafulila anasema, “Nimeendera kupinga utawala mbovu wa mkuu wa wilaya bungeni mpaka nishtakiwa polisi kwa kuwatetea wananchi wangu kutokana na vitendo vya mkuu wa wilaya kuchoma nyumba za wakulima.”

“Nimewapigania wananchi wangu hasa ukanda wa ziwa kwa kuitwa wakimbizi na serikali hii. Nilipambana mbele ya waziri mkuu na kuwatoa katika vizuizi wakazi wengi waliokamatawa. Nilirudishaia hadhi na heshima yao,” ameeleza Kafulila.

error: Content is protected !!