July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kafulila aikaba koo serikali

Mbunge wa KIgoma Kusini, David Kafulila

Spread the love

HOJA tatu za Msemaji wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Viwanda na Biashara, David Kafulila, zimeinyima raha serikali, huku Naibu Waziri, Janet Mbene akilazimika kumkejeli kwamba atafute ajenda nyingine sasa. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Kafulila ni muasisi wa hoja ya ufisadi wa uchwotwaji wa mabilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow ambayo imengo’oa vigogo kadhaa wa serikali.

Hoja hizo ameziibua leo wakati akisoma maoni ya kambi ya upinzani kuhusu muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mfumo wa stakabadhi ghalani ya mwaka 2013.

Katika hoja ya kwanza, Kafulila ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), amegusia kampuni za simu na migodi kuzuia serikali kuandaa kanuni za kutekeleza sheria zilizopitishwa na Bunge tangu 2010 kwa kuwa zinabanana na kampuni hizo na migodi ili nchi ipate kodi sahihi.

Anasema, “mwaka 2010, Bunge lilipitisha sheria (Postal&Telecom Act 2010) kutaka kampuni za simu zisajiliwe kwenye soko la mitaji Tanzania (Dar Stock of Exchange DSE)”.

Kafulila anasema lengo la sheria hii ilikuwa, kusaidia serikali kujua faida ambazo kampuni zinapata kwani kwa sheria hii mapato na matumizi yanakuwa wazi. Hivyo serikali ingepata kodi sahihi tofauti na ilivyo sasa.

“Ingesaidia wananchi kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hizo kwakuwa wangenunua hisa. Kama ilivyo Kenya ambapo kampuni ya SAFARI COM inamilikiwa na wakenya kupitia ununuzi wa hisa,”amesema.

Kuhusu migodi, amesema kuwa, mwaka huohuo 2010, Bunge lilipitisha sheria ya madini ambayo ilikuwa utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya Boman. Sheria iliItwa Mining Act 2010. Moja ya lengo kuu ilikuwa ni kutaka migodi isajiliwe kwenye soko la mitaji kwa faida hizi;

Kafulila anasema serikali ingepata kodi sahihi kwa kuwa mapato na matumizi ya migodi ingefahamika hivyo faida ingejulikana na serikali ingepata kodi sahihi tofauti na ilivyo sasa.

“Wananchi wangekuwa sehemu ya wamiliki kwa kununua hisa kama ilivyo Zambia ambapo kupitia kampuni ya Zambia Consolidating Company for Mining-ZCCM). Takribani Wazambia milioni na nusu wanamiliki migodi ya Zambia.

Kafulila amesema, “kwa mujibu wa taratibu, Bunge likishapitisha sheria inatakiwa wizara ziandae kanuni kutekeleza sheria. Sasa kwasababu sheria hizo mbili zinayabana makampuni ya simu ambayo yana pesa na migodi ambayo inapesa migodi na kampuni hizo zimegoma na yanatumia rushwa ndio sababu miaka yote tangu 2010 mpaka sasa wizara ya nishati na madini na wizara ya mawasiliano mawaziri wameshindwa kuandika kanuni.

“Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alishindwa, Prof. Muhongo akashindwa na hata sasa Boniface Simbachawene hakuna atachofanya”.

Anasema kwenye wizara ya mawasiliano Prof. Makame Mbawala ambaye ni waziri ni yaleyale hataweza kuandika kanuni kwani ameshashindwa miaka yote.

“Ndio msingi wa hoja yangu kutaka kanuni za kurekebisha sheria ya stakabadhi gharani zikamilike mara moja tusingie kwenye uzembe kama huo na zaidi sheria ya Commodity Exchange Markrt ikamilishwe.

“Nimesisitiza kwamba sheria ya masoko ya mazao (commodity exchange market) inapaswa kuletwa ili kuondoa genge la wafanyabiashara wa mazao ambao wanalangua mazao ya wakulima kupitia mfumo wa stakabadhi gharan na ulanguaji wa moja kwa moja,” amesema.

Kafulila amesema sheria ya masoko ya mazao ikiletwa itasaidia wanunuzi wote duniani kushindana kwenye ununuzi wa mazao tofauti na ilivyo sasa ambapo genge dogo la wafanyabiashara ndio linadhibiti soko.

“Nimesisitiza kwamba sheria hii hailetwi mapema kwa sababu ya ufisadi kwani wafanyabiashara wanaonufaika na hali ya sasa ndio wanahonga bodi za mazao na serikali kwa ujumla.

“Ndio mana mchakato wa kuandika sheria ulianza 2006 lakini mpaka leo haujakamilika. Ethiopia walianza nyuma yetu walishamaliza na sheria wanayo sisi tunaenda kujifunza namna wanavotekeleza hii ni aibu na ndio msingi wa kusema serikali imewekwa mfukoni na wafanyabiashara wasiowaminifu na makampuni.

error: Content is protected !!