January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kafulila achukuliwa fomu ya Ubunge

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila

Spread the love

DAVID Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) anatarajiwa kupewa zawadi Sh. 5 milioni na Mtandao wa kampeni ya ” IPTL – Bring Back Our Money”. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Baraka Mfilinge, Mratibu wa kampeni hiyo amesema zawadi hiyo inatokana na Kafulila kwa ujasiri kuibua na kupeleka bungeni ufisadi uliohusu “ukwapuaji fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow kiasi cha Sh. 360 bilioni.”

“Lengo la kumpongeza na kumshukuru Kafulila ni kwa sababu ya ujasiri na uzalendo wake kwa kuamua kupambana na mafisadi mpaka kufikia hatua ya sasa. Amepitia mengi ikiwemo vitisho na kejeli mpaka kupelekea kuitwa Tumbili,” amesema Mfilinge.

Mfilinge ameongeza kuwa: “Sisi kama Watanzania wazalendo na bila kujali itikadi zetu ila mapenzi kwa taifa letu, na kwa hiari yetu  tumeamua kuchangisha Sh. 5 milioni na fedha hizo tutazitumia kwenda kumchukua fomu ya ubunge ili Kafulila arudi katika bunge la 11 kuendeleza mapambano yake.”

Aidha, mtandao huo umetoa pongezi kwa wananchi na mashirika ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu.

Hivi karibuni mashirika hayo yalimpa Kafulila tuzo ya ujasiri na uzalendo kwa taifa na kuendelea kumpa msaada wa kisheria wakati wa mjadala wa Escrow na hata baada ya kufunguliwa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania na IPTL, PAP na Harbinder Singh Sethi kwa madai Kafulila aliwachafue hivyo wamlipe Sh. 300 bilioni.

“Tunaomba kuendelea kusisitiza kuwa ajenda ya kupambana na ufisadi na mafisadi ni yetu sote, hivyo basi ni vyema tukashirikiana ili pia ukweli kuhusu suala la mabehewa feki yaliyoligharimu taifa Sh. 238 bilioni ufahamike kwa ufasaha kwa watanzania,” amesisitiza Mfilinge.

error: Content is protected !!