February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kadi zawaondoa Fei Toto, Bocco mchezo wa Simba, Yanga

Spread the love

KUELEKEA mchezo utakaowakutanisha watani wajadi Simba na Yanga, Septemba 30, 2018 wachezaji tegemeo kwa vikosi vyote viwili Feisal Salumu ‘Fei Toto’ wa Yanga na John Bocco wa Simba hawatakuwa sehemu ya mchezo huo kutokana na kukabiliwa na adhabu za kadi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Bocco ataukosa mchezo huo kutokana na kuoneshewa kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC baada ya kumpiga ngumi beki wa timu hiyo na hivyo atakaa nje kwa michezo mitatu huku kwa upande wa Fei Toto ataukosa mchezo huo baada ya kuwa na kadi tatu za njano.

Wakati joto la mpambano huo likiendelea kupanda klabu Simba inatarajiwa kwenda kuweka kambi yake visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo, huku kwa upande wa mahasimu wao Yanga wanatarajiwa kujikita mkoani Morogoro kwa ajiri ya kufanya maandalizi.

Klabu hizo mbili zinaingia kwenye mchezo huo huku kila moja ikiwa imeshinda mchezo wake wa mwisho wa ligi, Yanga imeizidi Simba kwa tofauti ya alama mbili tu baada ya kushinda mechi zake zote nne za awali.

error: Content is protected !!