Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kada wa Chadema aliyesota rumande apata dhamana
Habari za SiasaTangulizi

Kada wa Chadema aliyesota rumande apata dhamana

Nyundo ya Hakimu
Spread the love

KADA wa Chadema wiyani Chato, Obadiah Kiko (41), amepanidhishwa kizimbani jijini Dar es Salaam akituhumiwa kuchapisha “taarifa za uongo juu ya serikali,” anaandika Faki Sosi.

Ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Obadiah alidaiwa kuchapisha taarifa kuhusu mazungumzo kati ya serikali na kampuni ya madini ya Acacia.

Akisoma mashitaka hayo, mbele ya Hakimu Makazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri, wakili mkuu wa serikali, Alex Masaba alisema, Obadiah alitenda kosa hilo, tarehe 3 Agosti mwaka huu. Masaba amedai kuwa Obadiah alitenda kosa hilo, akiwa Chato mkoani Geita.

Aliandika kwenye mtandao wa kijamii Facebook kuwa: “taarifa kutoka kikoa cha mazungumzo ya kati ya serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia… wanasheria wetu wanashindwa kutafsiri baadhi ya vifungu vya sheria hadi kufika kuomba msaada kwa wanasheria wa Acacia.

“Sasa huoni kuwa ni vituko mazungumzo yanaendelea wanasheria wetu wamebanwa sana ukizingatia wale jamaa wanavielelezo vyote vya mikataba….. serikali ikitaka kuvunja mkataba na Acacia Gharama kubwa zitatuusu.”

Lakini pia kuendekeza Uvyama itatughalimu saana baada ya Mheshimiwa Rais Magufuli angewashirikisha wakina mawakili wasomi waliokwiva kama wakili Tundu Lissu, Kibatala na Fatma Karume.

Kwenye mambo muhimu kama haya yeye kuleta uchama sasa itatugharimu //DictetaMagufulimustgo”.

Mtuhimiwa huyo aliyewakilishwa na wakili Peter Kibatala amedhaminiwa na wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya milioni 5.

Kesi hiyi itatajwa tena tarehe 16 Oktoba mwaka huu. Obadiah amekuwa rumande ya polisi kwa muda wa zaidi ya miezi miwili.

Taarifa zake kuwa amekamatwa na anashikiliwa na jeshi la polisi zilitolewa kwa mara ya kwanza hadharani na Lissu, siku tatu kabla ya kuvamiwa na kupigwa risasi mkoani Dodoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

error: Content is protected !!