Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kada wa Chadema aibua mapya kesi ya Mbowe wenzake
Habari za Siasa

Kada wa Chadema aibua mapya kesi ya Mbowe wenzake

Spread the love

 

LEMBRUS Mchome, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) mkoani Kilimanjaro, ameieleza Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, kuwa Askari Mpelelezi namba H4323 Msemwa, hakuwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam mwaka 2020,  kama alivyodai wakati anatoa ushahidi wake katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na wenzake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mchome ametoa madai hayo leo Jumatatu, tarehe 29 Novemba 2021, mahakamani hapo mbele ya Jaji Joachim Tiganga wakati akitoa ushahidi wake katika kesi ndogo ya kupinga maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu, Mohammed Abdillah Ling’wenya, yasipokelewe kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake.

Akiongozwa kutoa ushahidi wake na Wakili Fredrick Kihwelo, Mchome amedai baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, tarehe 11 Novemba 2020, kwa kosa la kupiga picha gari ya kiongozi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Mchome amedai kuwa, aliwekwa katika Kituo cha Polisi cha Mwanga, kisha akahamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Moshi, hadi tarehe 14 Novemba 2020, majira ya mchana aliposafirishwa kuelekea Dar es Salaam.

Kada huyo wa Chadema amedai kuwa, alipofika Dar es Salaam muda wa usiku, alifikishwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay, alifikishwa kaunta ambapo aliandikiwa maelezo yake na Askari Msemwa, kisha akapelekwa mahabusu kituoni hapo.

Fuatilia mahojiano ya Wakili Kihwelo na Mchome;

Kihwelo: Umefika Dar es Salaam maeneo gani?

Shahidi:Tulifikia Kituo cha Polisi Oysterbay.

Kihwelo: Askari ambao mlikuwa mmeambatana nao walikuwa wamebeba nini shahidi?

Shahidi: Walikuwa na silaha

Kihwelo: Walipofika Oysterbay walifanya nini?

Shahidi: Cha kwanza walinikabidhi kituoni kisha na wao wakakbidhi silaha walizokuwa nazo.

Kihwelo: Walikabidhi kwa nani kituoni hapo?

Shahidi: Walivikabidhi pale kaunta kulikuwa na askari yuko pale akachukua maelezo yangu akajaza kwenye kitabu cha kummbkumbu.

Kihwelo: Askari huyo alikuwa anaitwa nani?

Shahidi: Nilikuja kumfahamu jina baadae anaitwa Msemwa.

Kihwelo: Baada ya kukupokea nini kiliendelea tena?

Shahidi:Baada ya kunipokea niliwekwa mahabusu ambayo ni underground.

Kibwelo: Askari huyo aliyekupokea ulijuaje anaitwa Msemwa?

Shahidi: Sababu nilikaa naye muda mrefu hata beji yake kifuani ilikuwa imeandikwa Msemwa.

Kihwelo: Umesema mlitoka Kilimanjaro tarehe 14 Mei 2020 na kufika Dar es Salaam usiku,  ilikuwa tarehe ngapi ulivyofika?

Sbahidi: Tarehe 14

Kihwelo: Wale askari waliokufikisha Oysterbay walikwenda wapi?

Shahidi: Sikuwaona tena.

Kihwelo: Umekaa Polisi Oysterbay umekaa  ulikutana naye (Msemwa) mara ngapi?

Shahidi: Nimekutana naye mara nyingi sababu kila shift yake ilikuwa ikifika lazima tuonane.

Kihwelo: Umesema baada ya Oystebay ukapelekwa mahakamani kwa ijili gani?

Shahidi: Kesi iliyokuwa imefunguliwa.

Kihwelo: Nani alikuwa anaisimamia kesi zako?

Shahidi: Alikuwa ni Wakili Peter Kibatala.

Kihwelo: Nini hatima ya kesi yako?

Shahidi: Tarehe 2 Juni nilirudishwa mahakamani,  hakimu aligoma kunipokea akisema alitoa oda nipelekwe mahabusu Keko lakini sijapelekwa  na anashangaa Jeshi la Magereza halina taarifa zangu. Kwa hiyo tarehe 2 akawa amegoma kunipokea mahakamani.

Kihwelo: Imekuwaje mpaka umejikuta uko mahakamaani hapa?

Shahidi: Nilikuwa nafuatilia kesi hii, nikaona bwana Msemwa amekuja kutoa ushahidi na kuiambia mahakama hii tukufu kwamba mwaka jana alikuwa Central Polisi Dar es Salaam na kwamba amehamishiwa Oysterbay mwaka huu mwezi wa kwanza.

Kihwelo: Mwaka jana tarehe gani uliona alisema?

Shahidi: Sina kumbukumbu nzuri.

Kihwelo: Anakwambia alianza kufanya kazi Oysterbay Polisi mwaka huu mwezi gani?

Shahidi: Wa kwanza.

Kihwwlo: Baada ya kusikia hayo ulifanya nini?

Shahidi: Niliongea na aliyekuwa wakili wangu Peter Kibatala, nimemweleza hayo kwamba huyu mtu 2020 alikuwa Oysterbay na wala sio central kama alivyoeleza.

Kihwelo: Unamaanisha mwaka gani tarehe ipi?

Shahidi: Namaanisha mwaka jana Mei, kuanzia tarehe 14 nilimueleza hivyo akanihoji akanitaka nije Dar es Salaam na ikawa nimemwomba aandike barua kwenda Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuomba karatasi ya mashtaka, vilevile kuomba mwenendo wa kesi yangu baada ya kukubaliana hivyo nikaja Dar es Salaam,  siku ya tarehe 24 Novemba 2021.

Kihwelo: Nini kiliendelea?

Shahidi: Baada ya kufika kesho yake tarehe 25 Novemba nikaonana na Kibatala asubuhi, akawa ameniunganisha na mtu anayefanya kazi kwenye ofisi yake ambaye anaitwa Faith.

Akanipatia barua ambayo imeandikwa na Wakili Peter Kibatala kwenda Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuomba mwenendo wa kesi na hati ya mshtaka.

Kihwelo: Mlipofika Kisutu ulikutana

na nani ukiwa na Faith?

Shahidi: Tulienda chumba namba tano nikakutana na mama mmoja nikampa barua inatoka kwa wakili wangu akaoanisha barua ambayo tayari ameshaipokea na akaipokea kwa dispach akaiunganisha na barua zote mbili.

Kihwelo: Ameipoeka barua na kusaini dispach nini kiliendelea?

Shahidi: Alijiridhisha maombi aliyoleta ndiyo hayo hayo kwenye barua yangu lakini pia akajiridhisha kwamba ndiyo mimi.

Kihwelo: Hiyo barua iliainisha alitoa wapi na wewe ulitoa wapi?

Shahidi: Barua iliyokuwa imeandikwa na Kibatala iliyofikishwa pale na mimi nikapatiwa na Peter.

Kihwelo: Baada ya hapo akafanya nini?

Shahidi: Alinirudishia barua yangu,  ile nakala yangu akanipatia,  mwenendo wa kesi na hati ya mshtaka ambayo ilikuwa ni copied.

Kihwelo: Barua ya mashtaka ilikuwa copied?

Shahidi: Nilimhoji yule mama kwa nini ananipa copy sio original? Akaniambia kwa wakati huo hiyo ndiyo ilikuwa kwenye faili kwa hiyo niichukue haina shida yoyote.

Kihwelo: Pamoja na barua ya mashtaka nini ulikabidhiwa?

Shahidi: Mwenedo wa kesi

Kihwelo: Nini kiliendela?

Shahidi: Baada ya kukabidhiwa tulitoka na Faith tukaja mahakamni moja kwa moja mapokezi,  tukakutana na afisa wa mahakama tukampatia barua ambayo ilikuwa inatoka kwa Wakili Kibatala kwenda Kisutu kuomba mwenendo wa kesi na hati ya mshtaka.

Kihwelo: Baada ya kuwakabidhi walifanya nini?

Shahidi: Baada ya kukabidhi walipitia zote kwa pamoja, baada ya kuzipitia wakagonga mhuri kwenye copy yangu. Mimi wakanirudishia barua yangu ikiwa na mhuri wa mahakama hii.

Kihwelo: Kwa nini waligonga mhuri kwenye copy yako wewe?

Shahidi: Ni kuonesha kwamba mahakama imepokea barua

Kihwelo: Kwa muda wote toka umeipokea barua yako, nakala kutoka kwa Kibatala,  nakala ya mashtaka, dispach na mwenendo wa mashtaka vitu hivi vilibaki na nani?

Shahidi: Kuanzia tarehe 25 Novemba 2021 mpaka leo hii nimekuwa na hivi vitu, barua,  mwenendo wa kesi, hati ya mashtaka lakini pamoja na dispach.

Baada ya kuulizwa maswali hayo, Wakili Kihwelo alimhoji kama anazitambua nyaraka hizo, ambapo alijibu akidai anazitambua.

Alipomaliza zoezi la kuzitambua, Wakili Kihwelo alimhoji anaiomba nini mahakama hiyo, ambapo amejibu akidai anaiomba ipokee kama kielelezo.

Wakili Kihwelo alimuuliza anataka kuionesha nini mahakama hiyo kupitia nyaraka hizo, Mchome amejibu akidai Kwamba ushahidi alioutoa Msemwa si ushahidi wa kweli sababu mwaka jana alikuwa yuko tayari Oysterbay, nimeyathibitisha haya baada ya kurudishwa Oysterbay mwaka jana Mei.”

Kufuatia ombi hilo, Jaji Tiganga aliahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumanne, kwa ajili ya upande wa utetezi kueleza kama wanakubali vipokelewe au wanapinga visipokelewe.

Mchome ametoa ushahidi huo baada ya Askari Msemwa, akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hilla, hivi karibuni, kudai kuwa 2020 alikuwa akifanya kazi katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam na kwamba ilivyofika Januari 2021 alihamishiwa Kituo cha Polisi Oysterbay.

Katika ushahidi wake, Askari Msemwa alidai kwamba, tarehe 7 Agosti 2021 akiwa msimamizi wa Chumba cha Mashtaka cha Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, alimpokea Ling’wenya na mwenzake na Adam Kasekwa, waliotokea katika Kituo Kikuu cha Polisi Moshi, Kilimanjaro, baada ya kukamatwa tarehe 5 Agosti mwaka jana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!