Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Kada wa Chadema afia vitani Ukraine, akitetea Urusi
Habari Mchanganyiko

Kada wa Chadema afia vitani Ukraine, akitetea Urusi

Nemes Raymond Tarimo
Spread the love

 

RAIA wa Tanzania, mwanachama mwandamizi na kada mashuhuri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tarimo Nemes Raymond, amefariki dunia akiwa vitani nchini Ukraine. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka kwa mmoja wana familia wake zinasema, Nemes kama ambavyo afahamika ndani ya Chadema, alifikwa na mauti, katika mji wa Bakhmut, nchini Ukraine, Oktoba mwaka jana.

Alikuwa akipigana begwa kwa bega na jeshi la Ukraine, kupitia kundi la mamluki la Wagner linalomilikiwa na tajiri wa Urusi, Yevgeny Prigozhin, swahiba wa karibu wa rais wan chi hiyo, Vladimir Putin.

Taarifa zinasema, Nemes alikuwa mwanafunzi nchini Urusi, lakini alikutwa na kosa la jinai lililopelekea kufungwa jela kabla ya kupewa ofa ya kujiunga na kundi hilo la Wagner, kusaidia harakati za Urusi kuishambulia Ukraine ambapo alikutwa na mauti.

Moja ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, inawaonyesha wanaume waliovalia sare za kijeshi, wakiwa wameshikilia mishumaa kuzunguka jeneza lake, huku picha, medali mbili na cheti vikiwa vimewekwa kwenye jeneza lililokuwa na bendera ya Wagner.

Kabla ya kukutwa na masahibu hayo, Nemes mara kwa mara alikuwa akija nchini na kushiriki harakati za kisiasa ndani ya Chadema.

Katika uchaguzi mkuu wa 2020, alikuwa mmoja wa makada wa chama hicho, waliojitosa kutaka mbio za kumrithi John John Mnyika, kwenye mbio za kuwania ubunge katika jimbo la Kibamba, ndani ya Chadema.

Alishindwa na Ernest Mgawe, aliyeteuliwa na Kamati Kuu (CC), kupeperusha bendera ya chama hicho. Baadaye akarejea tena Urusi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mwenezi wa Chadema, Kata ya Saranga, Mwalimu Omari ilieleza kuwa chama hicho, kimepokea taarifa za kifo cha Nemes kwa majonzi makubwa.

Alisema: Ninasikitika kuwatangazia kifo cha mpiganaji mwenzetu ndani ya Chadema, kamanda Nemes Tarimo ambaye mwaka 2020, alikuwa ni mingoni mwa wagombea wa nafasi ya ubunge ndani ya chama.

“Alishika nafasi ya pili kati ya wagombea watatu, akitanguliwa na mheshimiwa Mgawe aliyepitishwa na mkutano mkuu maalum wa jimbo, uliofanyika katika ukumbi wa Victoria Genesis.”

Aliongeza, “marehemu Nemes amefikwa na umauti wakati akiwa katika majukumu yake ya kazi nchini Urusi, kama afisa katika taasisi moja yakimataifa inayojishughulisha na utoaji misaada kwa jamii.

“Hivyo kupitia machafuko ya vita baina ya Urusi na Ukraien, kamanda na mpiganaji huyu tumempoteza. Hakika vita aliyoipigana ndani ya chama chetu na hususana jimbo la Kibamba na kipekee wana wa Saranga haitafutika. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina.”

Hata hivyo, wakati Chadema wakisema, Nemes alikuwa akifanya kazi mashirika ya kutoa misaada, taarifa nyingine zinaeleza kuwa alikuwa mmoja wa mamluki wa Urusi.

Aidha, taarifa nyingine zinadai, Nemes alikuwa mwanafunzi nchini Urusi, aliyeajiriwa na kundi la Wagner kutoka gerezani alikokuwa amefungwa.

Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na serikali ya Tanzania wala Chadema, ambacho katika siku za karibuni kimekuwa na mahusiano mazuri na seikali, kuhusiana na “sakata hilo.”

Septemba mwaka jana, raia moja wa Zambia, alifariki nchini Ukraine alipokuwa akipigania Wagner, huku “Warusi Weusi” kadhaa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaaminika kuajiriwa na kampuni hiyo ya kijeshi.

Tarehe 1 Januari, mwanzilishi wa Wagner, Yevgeny Prigozhin alimsifu mamluki kutoka Cote d’Ivoire, ambaye alijiunga na mapigano nchini Ukraine.

Lemekhani Nyirenda, mwanafunzi wa Zambia mwenye umri wa miaka 23, alikuwa ameandikishwa kuipigania Urusi nchini Ukraine, kutokea gerezani.

Anadaiwa alikuwa akitumikia kifungo kinachohusiana na dawa za kulevya nchini Urusi, lakini aliachiliwa na kupelekwa mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine.

Aliuawa Septemba mwaka jana, lakini mamlaka ya Urusi ilikuwa imeifahamisha Zambia kuhusu kifo hicho, Desemba mwaka jana.

Kundi la Wagner, lilianzishwa mwaka 2014 na Prigozhin, na inaaminika kuwa linachukua takriban 10 asilimia ya vikosi vya Urusi nchini Ukraine, na limefanya operesheni huko Syria, Libya na Mali.

Kundi hilo, na mbinu zake mara nyingi zisizo za ubinadamu, sasa linajulikana kimataifa. Lakini habari kuhusu jinsi linavyofanya kazi na jinsi linavyofadhiliwa imebaki siri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!