December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kada Chadema auawa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto

Spread the love

ASIA Said, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), Kata ya Palanga, wilayani Chemba, Dodoma ameuawa kwa kupigwa na mshale. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mauaji hayo yalitokea jana jioni tarehe 22 Julai 2020, nyumbani kwa marehemu Asia, maeneo ya Palanga wilayani humo.

Akizungumzia tukio hilo, RPC Giles Muroto, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma amesema, chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro baina ya mume wa marehemu huyo, na mtu aliyetekeleza mauaji hayo.

Kamanda Muroto ameeleza kuwa, chanzo cha mgogoro huo ni mume wa marehemu kuingiza mifugo kwenye shamba la mtuhumiwa wa mauaji hayo.

Juma Omary, Kaimu Afisa Habari wa Chadema Kanda ya Kati amesema mtuhumiwa aliyemtaja kwa jina la Haruna Kimaki na mume wa marehemu walikuwa wanagombania sehemu ya malisho.

Omary amedai kuwa, mtuhumiwa lidhamiria kumuuwa mume wa marehemu, lakini mshale huo ulimpata mke wake na kumsababishia kifo.

“Chanzo Cha Tukio Hilo Ni ugomvi wa sehemu ya Malisho ambao ulimuhusisha mume wa Asia pamoja na  mfugaji ambae alifahamika kwa Jina la Haruna Kimaki.

Baada ya uchunguzi awali  kufanyika aliehusika na mauaji hayo alidhamiria kumuua  mume, lakini  Mshale huo ulimpata Asia nakusamsababishia umauti,” amesema Omary.

Omary amesema mazishi ya mwenyekiti huyo wa Bawacha Kata ya Palanga, yatafanyika leo Alhamisi tarehe 23 Julai 2020.

error: Content is protected !!