Sunday , 25 February 2024
Home Kitengo Biashara Kaboyoka alipigia chapuo zao la tangawizi
Biashara

Kaboyoka alipigia chapuo zao la tangawizi

Spread the love

MBUNGE wa Same Mashariki, Nagenjwa Kaboyoka (Chadema) ameitaka serikali kutoa kutangaza bei elekezi kwa wakulima wa tangawizi kutokana na wakulima wengi wa tangawizi kuibiwa kwa kuuza kwa bei ya chini, anaandika Dany Tibason.

Kaboyoka ametoa kauli hiyo leo Bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kutaka kujua serikali ina mkakati gani wa kupanga bei elekezi kwa wakulima wa Moshi Mashariki kutoka na kuwa wakulima wakubwa wa tangawizi .

“Kwa kuwa wananchi wa Same Mashariki ni wakulima wazuri wa tangawizi na sasa kiwanda cha tangawizi kimeharibika kwa muda wa miaka mitano sasa,lakini wakulima wamekuwa wakiuza tangawizi kwa bei ya hasara je ni lini serikali itatoa bei elekezi ili wakulima hao wasiendelee kuuza tangawizi kwa bei ya chini” alihoji.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Kyerwa Innocent Bilakwete (CCM) alitaka kujua Serikali imefikia hatua wapi katika kuondoa ushuru na kodi zinazomfanya mkulima asione faida kuendelea na zao la kahawa.

Kama serikali haiku tayari kuondoa tozo na kodi je,iko tayari kuwaruhusu wakulima wauze zao hilo kule ambapo wataona wanauza kwa bei nzuri.

“Zao la kahawa ni miongoni mwa zao kuu la biashara lakini bei yake imekuwa ni ya kukatisha tama kitu ambacho kinasababisha wengine kung’oa na kuikata kabisa kwa sababu nchini mwetu bei ni bado sana ukilinganisha na majirani yetu wa Uganda na wakati wa kampeini ua Rais Dk.John  Magufuli alihaidi kuondoa tozo zote pamoja na kodi zinazomkandamiza mkulima wa kahawa.

“Serikali imefikia hatua wapi katika kuondoa ushuru na kodi zinazomfanya mkulima asione faida kuendelea na zao la kahawa.

“Kama serikali haiku tayari kuondoa tozo na kodi je,iko tayari kuwaruhusu wakulima wauze zao hilo kule ambapo wataona wanauza kwa bei nzuri” alihoji Bilakwete.

Akijibu swali la Nyongeza la Kaboyoka, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha, amesema  kwa sasa Serikali ipo mbioni kufanya ukarabati na kufufua kiwanda cha tangawizi kilichopo Same Mashariki kwa lengo la kutaka wakulima kuuza tangawizi kwa bei nzuri.

Aidha amesema serikali kwa sasa inafanya uchambuzi wa kina na kubaini baadhi ya tozo, ada na ushuru unaotozwa kwenye mazao ya biashara haukuwa na mahusiano na uendelezaji wa mazao.

Amesema kutokana na hali hiyo serikali imeondoa jumla ya tozo 80 na kupunguza viwango tozo 4 katika tasinia ya mazao pekee kati ya jumla ya tozo 139 zilizopo.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Meridianbet yaimarisha usafi Kijitonyama

Spread the loveMABINGWA wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet leo imefanikiwa kufika...

Biashara

Kampeni SBL ya unywaji pombe chini ya umri yafika Kilimanjaro

Spread the loveKAMPUNI ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) inewahimiza wanafunzi...

Biashara

Cheza Pragmatic Play na ushinde mgao wa Bil 12 za Meridianbet kasino

Spread the love  HII habari njema kwa wapenzi wote wa michezo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mitaala yaandaliwa kukabili uhaba wa watalaam uchimbaji chini ya ardhi

Spread the loveKATIKA kukabiliana na uhaba wa watalaam wa uchimbaji  wa kina...

error: Content is protected !!