April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kabendera kupandishwa kizimbani

Erick Kabendera

Spread the love

MWANDISHI wa Habari, Erick Kabendera kesho tarehe 1 Agosti 2019 anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kabendera anayetuhumiwa kuwa sio raia wa Tanzania, atapandishwa kizimbani hapo kesho majira ya saa tatu asubuhi. Baada ya Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu (THRDC) kupitia mawakili wake, kufungua maombi ya dhamana Namba 14 ya mwaka 2019.

Kabendera anatetewa na Mawakili Jones Sendodo, Shilinde Swedy na Catherine Ringo kutoka mtandao wa THRDC.

Loy Kabendera mke wa Kabendera leo tarehe 31 Julai 2019 ameruhusiwa kumuona mume wake ikiwa zimepita siku mbili tangu alipokamatwa na jeshi la Polisi tarehe 29 Julai mwaka huu, akiwa nyumbani kwake Mbweni Jijini Dar es salaaam.

Kwa mujibu wa THRDC, Kanbendera anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilwa Road.

error: Content is protected !!