April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Kabendera hajamalizana na DPP’

Mwandishi Erick Kabendera akiwa mahakamani

Spread the love

ERICK Kabendera, mwandishi wa habari za uchunguzi nchini, bado yupo kwenye majadiliano na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Makosa ya Jinai (DPP). Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 27 Januari 2020 na Gloria Mwenda, Wakili wa Serikali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakati shauri la kesi hiyo lilipoitwa. Katika kesi hiyo, Kabendera anashitakiwa kwa makosa matatu likiwemo uhujumu uchumi.

Wakili Mwenda ameiombia mahakama kupanga tarehe nyingine kwa kuwa, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika huku majadiliano kati ya mshtakiwa na DPP yakiendelea. Kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 10 Februari 2020.

Katika shtaka la kwanza anadaiwa katika kipindi hicho, alijihusisha  na mtandao wa uhalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Shtaka la pili anadaiwa katika kipindi hicho bila ya sababu alikwepa kodi ya Sh173.2 milioni aliyotakiwa kulipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la tatu, anadaiwa kutakatisha Sh173.2 milioni huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na utakatishaji fedha.

error: Content is protected !!