August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JWTZ yafura, yalionya gazeti

Spread the love

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limechukizwa na kitendo cha gazeti la Tanzania Daima kulihusisha jeshi hilo na ushiriki wake katika propaganda za kisiasa, anaandika Charles William.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi wa Mahusiano ya jeshi hilo makao makuu jioni ya leo, imeeleza kuwa, JWTZ imesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti hilotoleo Na. 4290 la tarehe 01 Septemba mwaka huu.

“Jeshi ni taasisi ya dola wala si taasisi ya kiitikadi, kwa maana uhusiano wake na wanasiasa ni wakati linapotetea na kulinda maslahi ya wananchi, Jana tulikuwa tunasherekea kuzaliwa kwa JWTZ, ieleweke hivyo na iachwe mara moja kuchanganywa na mambo ya siasa,” Imeeleza taarifa hiyo.

error: Content is protected !!