May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Julio na ‘wanae’ kibaruani dhidi ya Ghana

Spread the love

 

TIMU ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes) ambayo ipo chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ itakuwa na kibarua cha kuikabili timu ya Taifa ya Ghana, kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa kundi C, utapigwa majira ya saa 1 usiku kwa saa Afrika Mashariki, kwenye Uwanja wa Olympic uliopo kwenye mji wa Nouakchott nchini Mauritania ambapo michuano hiyo inafanyika.

Kuelekea kwenye mechi hiyo, kocha wa kikosi hiko Julio amesema kuwa wameiangalia timu ya Ghana kwa njia ya mkanda wa video na kuona mapungufu yaona watahakikisha wanafanya vizuri kwenye mchezo wa leo licha ya kuwa na uchanga kwenye michuano.

“Tunacheza mechi ngumu kwa kuwa tunacheza na watu waliozoea mashindano, ila sisi tumejipanga vizuri na tumekuja kupambana kwa kufanya jambo ambalo watanzania wametutuma.

“Tumetumia muda wetu mimi pamoja na benchi langu la ufundi na tumegundua hawako vizuri kwenye upande wa kuzuia na tumeshaongea na vijana na tunaomba watanzania kutuombea, kwa vile sisi ni wachanga kwenye mashindano haya,” alisema Julio.

Michuano hiyo ilianza tarehe 14 Februari 2021, ambapo mpaka sasa imeshapigwa jumla ya michezo mitatu na kwenye mchezo wa ufunguzi mwenyeji alipoteza kwa bao 1-0, mbele ya Cameroon.

Ngorongoro Heroes ilifuzu michuano hiyo mara baada ya kushika nafasi ya pili kwenye michuano ya kombe la CECAFA, baada ya kupoteza kwenye mchezo wa fainali kwa mabao 4-1, mbele ya Uganda, jijini Arusha 2020.

error: Content is protected !!