May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Julio alia na wachezaji Stars, ataka wajiongeze

Jamhuri Kihwelu 'Julio'

Spread the love

 

KOCHA wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (NgorongoroHeroes), Jamhuri Julio amelia na namna ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kuwa walishindwa kujiongeza mpaka kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) baada ya kutoka sare ya mabao  2-2 na Guinea. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Taifa stars iliondolewa kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Cameroon baada ya kumaliza kwenye nafasi ya tatu kundi D, wakiwa na pointi nne.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari leo tarehe 1 Februari 2021, kocha huyo alisema kuwa wakati Stars inaongoza 2-1 dhidi ya Guinea wachezaji walipaswa kujiongeza na siyo kila kitu kumuachia kocha ili waweze kuibuka na ushindi.

“Tunaweza kuwaona makocha wabovu au hawafai, mwalimu anafundisha mbinu na ufundi kuna muda wachezaji wanatakiwa wabuni wenyewe kwa kujiongeza ili waweze kushinda lakini siyo kila kitu mwalimu apige kelele,” alisema Julio.

error: Content is protected !!