Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Jukwaa la vijana “GO na NMB” lazinduliwa Zanzibar, SMZ yapongeza
Habari Mchanganyiko

Jukwaa la vijana “GO na NMB” lazinduliwa Zanzibar, SMZ yapongeza

Spread the love

BENKI ya NMB nchini Tanzania imelizindua rasmi jukwaa la kuwawezesha vijana la “GO na NMB” Visiwani Zanzibar na kusema iko tayari kusaidia kuwajenga kiuchumi na kuwakwamua kifedha kwa kuwahudumia kidigitali, kuwakopesha na kuwapa elimu ya fedha. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taasisi hiyo kinara wa suluhishi za kifedha nchini imesema, inao uwezo wa kufanya hivyo kutokana na kuwa na nguvu stahiki kifedha na kuongoza sokoni kwa ubunifu wa hali ya juu.

NMB inasema imejipanga kikamilifu kuchangia kuwafanya vijana wa Zanizbar kuwa na nidhamu ya kutumia fedha ili wawe raia wanaowajibika vyema kifedha.

Benki hiyo iliweka bayana dhamira hiyo juzi Jumamosi tarehe 25 Juni 2022 Unguja wakati wa uzinduzi rasmi wa jukwaa la “GO na NMB” uliofanyika Forodhani ambapo ngeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Hemed Suleiman Abdulla, aliyesema uwekezaji huo ni chachu hitajika ya maendeleo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth zaipuna, Afisa Mkuu wa Biashara na wateja Binafsi, Filbert Mponzi (wa pili kutoka kulia) na Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Said Shaame na Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Simai Msaraka wakipiga makofi baada ya kuzinduliwa huduma ya Gon na NMB

Akiuelezea mpango huo wenye manufaa lukuki, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema benki hiyo iko pia vizuri kiteknolojia kusaidia kuyabadilisha maisha ya vijana wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Kwenye maelezo hayo, Zaipuna alibainisha jukwaa hilo la kuwawezesha vijana ni njia ya kufahamiana miongoni mwao huku lengo kuu likiwa kuwaandaa kuwa raia wenye tija kiuchumi na wanaojitambua kimaendeleo.

Aidha, alisema “GO na NMB” ni maalum kwa vijana na mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo kuboresha huduma zake na kuongeza mchango wa kisekta kwa makundi mbalimbali ili kuendelea kusaidia juhudi za Serikali za kukuza uchumi.

“Go na NMB” ni ubunifu wa hali ya juu wenye suluhishi za kidijitali kwa ajili ya kundi hili la jamii. Jukwaa hili linatoa fursa kwa vijana kutumia huduma zetu kwa manufaa yao ili waweze kutimiza ndoto na malengo ya maisha yao,” alisema Zaipuna

“Jukwaa tunalozindua linatoa suluhu kwa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya fedha. Linakuja na fursa nyingi hasa kwa vijana kama mikopo kama rasilimali fedha na bidhaa nyingine kama MastaBoda, Mastaboti na pia kutoa elimu ya kifedha.”

“Pia bidha zetu zimechakatwa vizuri ili kuboresha malipo ya kielektroniki na habari njema ni kwamba wateja wetu sasa wanaweza kupata mikopo ya papo kwa papo (Mshiko Fasta) kwa kutumia simu zao za mkononi bila kufika kwenye matawi yetu,” alisema.

Aidha, Zaipuna alisema jukwa hilo litawahamasisha vijana kujiwekea akiba na kuweka mikakati ya kuwa na shughuli za uzalishaji na kuwahakikishia vipato wakati wote, alibainisha.

“Lengo letu ni kuwavutia vijana kwenye jukwaa litakalo wajengea uwezo wa kujitegemea kwa kuwapatia suluhishi za mahitaji yao mbalimbali ya kifedha. Pia tunalenga kuwasaidia vijana kujenga nidhamu ya fedha wanapoandaa maisha yao ya baadae kitu ambacho tuna imani kitachangamsha uchumi wa nchi,” alisema Zaipuna

Alisema kuwahudumia vijana na kuwapa elimu ya fedha ni swala la msingi kutokana na wingi wao ambao sasa hivi ni asilimia 64 za watu wote nchini. Fursa za “GO na NMB” kwa vijana ni pamoja na mikopo ya vitendea kazi kama pikipiki (Mastaboda), mikopo ya boti (Mastaboat), kufahamu matumizi na faida za huduma za kidigitali kama NMB Lipa Mkononi, MshikoFasta na NMB Pesa Wakala.

Wakati huduma ya MshikoFasta inamwezesha kijana kukopa mpaka Sh.500,000 kidijitali bila kuwa na dhamana, NMB Pesa Wakala inatoa nafasi nyingi kwa vijana wengi kujiajiri kutokana na kulegezwa kwa masharti ya biashara hiyo.

Faida nyingine za “GO na NMB” ni pamoja na mafunzo ya programu za huduma jumuishi za kifedha, bima ya bure ya simu za mkononi na kupata fursa za ajira kupitia mafunzo ya usimamizi. Nyingine ni kupata fursa za kuhudhuria matukio mbalimbali kama makongamano ya wanafunzi vyuoni na fursa za mafunzo ya ujasiriamali.Katika hotuba yake, Makamu wa Rais, Abdulla alisema jukwaa hilo ni jambo jema linaloendana na juhudi za Serikali za kutatua changamoto zinazowakabili vijana na kuwashirikisha katika ujenzi wa taifa.

Alisema “GO na NMB” imekuja wakati muafaka na ni uwekezaji wenye tija kwa sababu kuwainua vijana kifedha na kiuchumi kutasaidia sana kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira. Umuhimu wa jukwaa hilo, aliongeza, pia unatokana na kuzingatia elimu ya masuala ya kifedha ambayo sasa hivi iko chini ya asilimia 30 na upatikanaji wa mitaji kirahisi.

“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua na kutoa kipaumbele katika kuendeleza vijana kwa dhamira ya kujenga uwezo wa kujitengemea kuliko kutegemea ajira kama chanzo cha mapato yao.

Kwa kuzindua mpango huu, vijana wataanza kutambua umuhimu wa kujiwekea akiba na pia kutumia teknolojia kujipatia faida mbalimbali ambazo kama wakitumiwa vizuri, zitasaidia kutengeneza ajira na hivyo kupunguza tatizo la ajira hapa visiwani,” alisema

“Nachukua nafasi hii kuwapongeza sana NMB kwa hatua hii mliyofikia katika kuhakikisha kuwa mnawakwamua vijana pale walipo na kukitengeneza vizuri kizazi hiki kiwe ni kile chenye nidhamu ya fedha.”

Naye Mkuu wa Wilaya ya Zanzibar Mjini, Rashid Simai Msaraka alisema jukwaa la GO na NMB limezinduliwa kwa wakati muafaka kwa kuwa wakazi wengi wa Zanzibar kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la wafanyabiashara ambao wanawakopesha fedha zao kwa riba kubwa mno huku akisema ujio wa GO na NMB utasaidia kutokomeza tatizo hilo.

“Wakazi wa Zanzibar wamekuwa wahanga wa mikopo lakini tumekuwa tukipokea watu wengi kwenye ofisi zetu wanaohitaji kupata mikopo. Hii imekuwa ikitufanya tukose usingizi nyakati fulani. Tunafurahi kwamba NMB imeanzisha bidhaa zinazoweza kutoa masuluhisho ya kifedha kwa viwango vya riba nafuu bila kupitia mifumo ya kibenki iliyozoeleka,” alisema

Jukwa la GO na NMB kwa mara ya kwanza lilizinduliwa jijini Dar es Salaam mwaka 2021 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!