Saturday , 3 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lazinduliwa
Habari Mchanganyiko

Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lazinduliwa

Spread the love

 

JUKWAA la kitaifa la kuwawezesha wanawake kiuchumi limezinduliwa ili kuliwezesha kundi hilo kufikia fursa zinazowazunguka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Uzinduzi huo umefanywa hivi karibuni jijini Dodoma na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, kwa kushirikiana na Taasisi ya Legal Services Facility.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, amesema jukwaa hilo limeanzishwa ili kuongeza uelewa kwa wanawake kuhusu masuala ya Biashara, upatikanaji mitaji na Sheria za nchi katika masuala ya uchumi.

Amesema mbali na jukwaa hilo la kitaifa, Serikali imeunda majukwaa ngazi ya mkoa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima

“Kupitia maazimio ya mkutano wa wanawake Beijing 1995, Tanzania iliamua kujikita katika maeneo manne ambayo ni: kuwawezesha wanawake kiuchumi; wanawake na haki za kisheria; usawa katika elimu, mafunzo na ajira; na wanawake katika nafasi za uongozi na ngazi za Maamuzi.”

Waziri huyo wa maendeleo ya Jamii amesema “pia, mwaka 2021, Tanzania ilishiriki Mkutano wa Kimataifa wa Jukwaa la Kizazi chenye Usawa (Generation Equality Forum) uliofanyika Jijini Paris – Ufaransa, ambapo Tanzania iliwasilisha ahadi za nchi, ambazo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ni kinara katika utekelezaji wa eneo linalohusu haki na Usawa wa Kiuchumi.”

Katika hatua nyingine, Dk. Gwajima ameyaagiza majukwaa hayo nchi nzima kuwaunganisha wanawake katika fursa za kibenki, masoko na utaalamu wa kuboresha uzalishaji wa bidhaa zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala

Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala, amesema Shirika hilo imeamua kushirikiana na Serikali katika uzinduzi wa jukwaa hilo, kwa kuwa linagusa moja ya maeneo muhimu ya utekelezaji wa programu ya upatikanaji wa haki kwa watu wote.

“Ni matumaini yetu kuwa Jukwaa hili la kitaifa litajikita katika kusghulikia changamoto mbalimbali za wanawake kwenye masuala ya kiuchumi, masuala ya kisera, kitaaluma, kirasilimali pamoja na haki nyingine za msingi za kiuchumi. Sisi kama LSF tutaendelea kushirikiana na Jukwaa hili kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,” amesema Ng’wanakilala.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!