January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jukata yamshauri Rais Kikwete

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) na Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein (katikati) wakionesha katiba Mpya

Spread the love

JUKWAA la Katiba Tanzania (JUKATA), limemtaka Rais Jakaya Kikwete kuielekeza serikali kuanza kuandaa miswada kwa ajili ya marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura namba 83, toleo la mwaka 2014 na Sheria ya Kura ya Maoni ya mwaka 2013. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Mbali na kuandaa miswada hiyo, Rais Kikwete ametakiwa kusimamia makubaliano ya Chamwino, Dodoma baada ya kukaa na wenyeviti wa vyama vya upinzani na kukubaliana kuhusu kufanya baadhi ya marekebisho kwenye Katiba ya mwaka 1977 kabla ya uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Hatua hiyo inakuja, baada ya sheria hizo kuisha muda wake kutokana na mkwamo uliopo kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda amesema vifungu vilivyopitwa na muda ni; kifungu cha 4 (1) kuhusu Rais kuiagiza NEC kuitisha kura ya maoni, kifungu cha 4 (3) kuhusu NEC kuchapisha swali la kura ya maoni na Kifungu cha 5 (1) kuhusu muda wa kuelimisha na kuhamaisha wananchi kupiga kura ya maoni.

“Vifungu vingine vilivyokwisha muda wake ni; Kifungu cha 5 (2) kuhusu muda wa kutoa taarifa kwa umma juu ya utaratibu wa kuendesha kura ya maoni, kifungu cha 5 (3) kuhusu siku 60 za kutoa elimu ya uraia,” amesema Mwakagenda.

Mwakagenda amevitaja vifungu vingine kuwa ni; kifungu cha 13 (1) kuhusu muda wa usajili wa kamati za kura ya maoni na kifungu cha 16 (1) kuhusu siku 30 za kampeni ya ndiyo au hapana kuhusu Katiba Inayopendekezwa.

“Rais anapaswa kuweka kuweka bayana lini kitafanyika nini. Pia anayo fursa ya kuelekeza serikali kuanza kuandaa miswada kwa ajili ya marekebisho ya sheria mbili zinazoongoza mchakato wa Katiba Mpya tayari kwa uwasilishaji bungeni katika mkutano utakaoanza Novemba mwaka huu,” amesema Mwakagenda.

Mbali na hayo, Mwakagenda amesema JUKATA imeaanda makubalino mengine yanayohusu mwendelezo wa mchakato wa Katiba Mpya baada ya uchaguzi mkuu ambapo wakati wowote watavitaka vyama vya siasa vyote kuweka sahihi na kufanya utekelezaji wake.

error: Content is protected !!