June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JUKATA: Serikali isiwaingilie NEC

Naibu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Hebrone Mwakagenda

Spread the love

SERIKALI imetakiwa kuacha kuingilia utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu daftari la kudumu la wapiga kura na kuilazimisha kuendesha kura ya maoni 30 Aprili. Anaandika Pendo Omary (endelea).

Badala yake imetakiwa itekeleze jukumu lake la kuwezesha upatikanaji wa fedha za kutosha kwa ajili ya uandikishwaji wa wapiga kura kwa ukamilifu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Hebron Mwakagenda – Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) amesema, “mchawi katika zoezi hili ni serikali. Rais Jakaya Kikwete alitangaza kura ya maoni itakuwa 30 Aprili. Sio kazi yake. Ameingilia utendaji wa NEC”.

Mpaka sasa serikali imenunua vifaa vya uandikishaji 250 kati ya 8000 ilivyoahidi huku mahitaji halisi yakiwa ni vifaa vifaa 26,000.

Mwakagenda amesema, kuendelea kulazimisha upigaji kura ya maoni 30 Aprili huku serikali ikishidwa kutoa fedha za kutosha kwa NEC kuendesha zoezi ikiwemo kununua vifaa vya uandikishwaji na kupigia kura kumepelekea yafuatayo;

Wananchi katika Mkoa wa Njombe kunakofanyika uandikishaji kutoa rushwa ili waandikishwe kwenye daftari la wapiga kura baada ya kusota kwenye foleni kwa siku tano bila kujiandikisha; kata zote tatu zenye wananchi wasiopungua 26,000 waliotakiwa kujiandikisha zilikuwa na mashine 36.

“Pia imepelelea wananchi wengine kususia kujiandikisha. Ufuatiliaji wa vituo vyote uliofanywa na JUKATA 18- 22 Machi mwaka huu, umeonesha hali bado ni tete, ” amesema Mwakagenda.

Ameongeza kuwa in Kata moja ya Yaboko ilionesha kukamilisha uandikishaji kwa asilimia 80 wakati kata zingine zikisuasua. Wananchi waliofanikiwa kujiandikisha mpaka 22 Machi kwa Kata tatu za Yakobi, Kifanya na Mjimwema ni 17,000 huku wananchi 9,000 wakisubiri kabla ya 12 Aprili kazi ya kuandikisha kumalizika katika maeneo hayo.

“Kwa hali ya sasa, Katiba inayopendekezwa haina tija. Haiwezi kuzaa katiba mpya. Mchakato wa kupata katiba mpya umekwama na kushindikana,” amesisitiza Mwakagenda.

Kutokana na mkwamo huo, serikali imetakiwa kutekeleza makubaliano ya Chamwino kati ya Rais na vyama vya siasa wanachama wa Kituoa cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuhusu mchakato katiba na uchaguzi mkuu wa mwaka huu ili kuleta amani na utengano nchini.

error: Content is protected !!