July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JUKATA kufunga Bunge Maalum la Katiba

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba

Spread the love

JUKWAA la Katiba Tanzania (JUKATA) limelitaka Bunge Maalum la Katiba kusitisha shughuri zake ndani ya wiki mbili kuanzia June 12, 2014, vinginevyo litahamasisha wananchi kuandamna na kwenda mkoani Dodoma kufunga rasmi ukumbi wa Bunge.

Deus Kimbamba, mwenyekiti wa JUKATA amewambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Tunatoa wiki mbili Bunge Maalum la Katiba liwe limesitisha shughuri zake. Vinginevyo, tutafika Dodoma kwa wingi wetu tukiwa na makufuli kwa ajili ya kufunga rasmi ukumbi wetu wa Bunge kama ishara ya kusitisha rasmi Bunge hilo lisiendelee kufuja pesa za walipa kodi wa Tanzania”

JUKATA inachukua hatua hiyo baada ya mkwamo wa mchakato wa katiba mpya ikiwemo hujuma inayofanywa na Mwenyekiti wa Bunge hilo Samuel Sitta na mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema kwa maslahi binafsi, kupuuzwa kwa rasimu iliyobeba maoni ya wananchi na kutokuwepo kwa maridhiano ya kisiasa.

error: Content is protected !!