Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Juhudi za kumkomboa mtoto wa kike ziendane na kumfikisha wa kiume kujitambua
Habari Mchanganyiko

Juhudi za kumkomboa mtoto wa kike ziendane na kumfikisha wa kiume kujitambua

Spread the love

 

MENEJA wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo Tanzania (SIDO) Mkoa wa Morogoro, Joan Nangawe anasema juhudi za kumkomboa mwanamke na kumtoa katika wimbi la umaskini sambamba na masuala ya usawa wa kijinsia ziendane na kumkomboa mwanaume kifikra ili kila mmoja ajitambue kwa nafasi yake ili kutorudi nyuma kwenye mfumo dume. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Anasema kwa sasa wanawake wanaongeza zaidi juhudi ya kujituma na kutafuta maendeleo ambapo wanaweza wakafika mahali na kuwadharau wanaume na kuona kwamba wao pia wanaweza kufanya mambo yao.

“Kila mmoja anapaswa kujitambua kwa nafasi yake, lakini mwanamke asije akajitambua saana na mwanaume akachelewa, itakuwa mfumo jike, sababu kwa sasa naona wanawake wanaenda na spidi kubwa ya maendeleo kutafuta, naonaa mwanamke anaweza akamdharau mwanaume,” anasema.

Hivyo anasema pamoja na kwamba mwanamke anapata elimu mbalimbali na kufikia kuwa na uwezo wa kufanya mambo bila kumtegemea mwanaume lakini pia mwanaume nae apewe nafasi ya kutambua mambo na kuyachanganua sambamba na mwanamke ili wote kwa pamoja kufikia kuzungumza lugha iliyo salama.

Aidha Nangawe anasema wanaume ni sehemu ya watoto wanaozaliwa na wanawake na wanapaswa kuelekezwa nini wafanye ili kila mmoja awe anatambua nafasi yake na kujenga jamii iliyo bora.

Anasema kizazi cha sasa ni tofauti kidogo na kizazi cha nyuma sababu kizazi cha nyuma kinajua masuala ya mfumo dume zaidi lakini cha sasa wengi huzaliwa na kulelewa na mama pekee (single Mothers) masuala ya baba hawayajui wakibaki kumshuhudia mama pekee akiwa na uwezo wa kuleta mahitaji nyumbani jambo litakaloleta athari ya kukariri kwa watoto wa kiume kwamba wajibu wa kulea nyumba ni wa mama jambo ambalo sio sahihi.

“sisi ni wazazi na tunazaa watoto wa kike na kiume sasa tukielekeza nguvu zaidi kuwaelimisha watoto wa kike tutabaki na watoto wa kiume ambao watashindwa kujihudumia baadae, watadhani wao wanapaswa kukaa tu na sio kuhudumia familia wakati kila mmoja anapaswa kuwajibika kwa nafasi yake” anasema Meneja huyo.

Hivyo anasema jamii ina wajibu wa kuwajenga watoto kila mmoja kutambua nafasi yake wa kike na kiume haijalishi nani atakuwa na uwezo wa kujitambua zaidi lakini nafasi ya mwanaume ibaki pale kwa maana ya haki na usawa wa pamoja.

Akizungumzia masuala ya mikopo Nangawe anawaasa wanawake kuacha kujiingiza kwenye mikopo umiza inayoweza kuwaletea umaskini baadae bali wakope huku wakijua namna ya matumizi ya mkopo na namna ya kurejesha mkopo husika.

Naye Mmoja wa wajasiriamali wanawake mkoani hapa Lilian Mgongolwa anasema Taasisi zinazohusiana na kuelimisha wanawake katika kuondokana na umaskini zipapaswa kuwawesha wanaume pia ili kuweka usawa na kumfanya mwanaume kujua mipaka yake na mwanamke ili kubadilisha mitazamo ya vijana wanayoiona ya mama kusaidia familia zao bali jukumu hilo ni la wote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!