July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jua laathiri matangazo ya setelaiti

Madishi ya setelaiti

Spread the love

MFUMO wa dunia kuwa karibu na jua umetajwa kuathiri matangazo ya setelaiti ambayo yanatumika kurusha matangazo ya televisheni. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Walker Wang – Mkurugenzi wa ufundi wa kampuni ya Star Media (Tanzania) Limited inayosambaza visimbuzi vya StarTimes.

Wang anatoa kauli hiyo kufuatia, kukatika mara kwa mara kwa matangazo.

Akizungumza na MwanaHALISIOnline leo, katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Wang amesema “yapo madhara ya jua kuwa karibu na dunia. Madhara haya hutokea mara mbili kila mwaka”.

Wang amesema, wakati dunia inalizunguka jua, hutokea vipindi viwili ambavyo jua huwa karibu na dunia. Hali hiyo husababisha mawimbi ya “hertzian” kuathiri Satelaiti ambazo hufanya kazi ya kupokea matangazo ya vituo vya televisheni.

“Katika mwaka vipindi hivi hutokea Machi na Septemba. Kila mwezi hutokea kwa siku 20 na katika kila siku hutokea kwa dakika 10 mfululizo hasa hasa muda wa saa tisa mchana. Hali hii huathri matangazo ya televisheni yanayorushwa kupitia setelaiti,” amefafanua Wang.

Aidha, Wang ameongeza kuwa matumizi ya antena zisizo na viwango pia husababisha matangazo ya televisheni kukatika au kugoma.

Amesema, kila wiki kampuni hiyo hutembelea wateja wao kwenye makazi yao na wamebaini asilimia 90 ya wateja wanatumia antena ambazo hazina ubora.

Aidha, Abdulkadir Mbeo – Naibu Mkurugezi wa ufundi wa kampuni hiyo, amesema suala lingine linalochangia kukatika na kugoma kwa matangazo kupitia ving’amuzi ni uandaji dhaifu wa matangazo katika vituo vya televisheni.

“Sisi tunapokea matangazo, hatuyaandai. Wakati mwingine matangazo yanayoandaliwa na vituo vya televisheni yanaweza kuwa na matatizo,” amesema Mbeo.

error: Content is protected !!