August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jua kupatwa Sept 1

Spread the love

CHUO Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kimetoa utafiti wa tukio la kupatwa kwa jua nchini pamoja na sehemu zote za Afrika pia Madagaska litakalotokea tarehe 1 Septemba mwaka huu, anaandika Faki Sosi.

Akizungumza na waandhishi wa habari leo Dk. Noorali Jiwaji, mtaalam wa masuala ya (astronomy) kutoka OUT amesema, tukio hilo litatokea kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana huku katika maeneo ya Kusini mwa Tanzania jua litapatwa kipete.

“Kupatwa kipete ni moja ya aina ya kupatwa kwa jua, jua likipatwa kipete linaonekana kama pete badala ya kuwa mviringo kwa kuangalia kutumia chujio maalum la mwanga,”amesema.

Amesema, Watanzania waliopo Mikoa ya Kusini wataona jua kama pete kwa dakika chache, wakati Watanzania wote pamoja na Kusini wataona jua limepatwa kihilali (kawaida) kwa masaa manane.

Pamoja na kutokea kwa tukio hilo amesema, watu wanatakiwa kajizuia kwa kutoangalia tukio kwa kutumia njia zingine ili kuona umbo la jua bali ni kwa kutumia kichuja nguvu ya jua (Polymer Filter) kinjachoagizwa kutoka marekani.

“Hadi sasa kampuni ya SBC Tanzania LTD, watengenezaji wa kinywaji cha Pepsi wameahidi kudhamini chujio 50,000 maalum za mwanga ili kuzisambaza mashuleni, pia wadau wengine wanakaribishwa kudhamini,” amesema.

error: Content is protected !!