Saturday , 22 June 2024
Home Habari Mchanganyiko JPM uso kwa uso na walimu
Habari MchanganyikoTangulizi

JPM uso kwa uso na walimu

Rais John Magufuli akizungumza
Spread the love

RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwa ngeni rasimi katika mkutano Mkuu wa kwanza wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Desemba 14 mwaka huu., anaandika Dany Tibason.

Mkutano huo itakuwa ni mara ya kwanza kwa mkuu huyo wa nchi kukutana na walimu tangu kuchaguliwa kwake kushika madaraka katika serikali ya awamu ya tano.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Dodoma, Augustine Njamasi amesema jambo kubwa ambalo walimu wanataka kuzungumza mbele ya rais Magufuli ni kutoa kilio chao cha miaka mingi cha walimu kutopata stahiki zao kwa wakati licha ya kuwa kada hiyo imekuwa kimya sana na hajaweza kuchukua maamuzi magumu.

Amesema walimu kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakilalamikia kutopata malipo yao ambayo ni malimbikizo ya mishahara,kupanda kwa madaraja ,malipo ya matibabu na malipo ya likizo.

“Kitendo cha kuwepo kwa rais katika mkutano huo mkuu wa walimu utazaa matunda kwani yatapatikana majibu sahihi na kwa wakati tofauti na miaka mingine ambayo walimu wamekuwa hawajui hatima ya madai yao ni lini yatalipwa,” amesema.

Pamoja na mambo mengine Njamasi amesema kuwa kitendo cha rais Magufuli kukubali kukutana na walimu ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu aingie madarakani kutawafanya walimu kujua hatima ya maisha yao ukizingatia kuwa pamoja na kwamba walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu lakini wamekuwa wakifanya kazi yao kwa uvumilivu mkubwa zaidi.

Mwenyekiti huyo wa CWT mkoa wa Dodoma amesema mpaka sasa maandalizi ya mkutano mkuu yamekamilika kwa asilimia tisini na nane na kueleza kuwa mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Chimwaga.

Amewaelezea wandishi wa habari kuwa mkutano huo utafanyika kuanzia Desemba 14 hadi 16 mwaka huu huku wajumbe wa mkutano wanatarajiwa kuwa na idadi ya wajumbe 3000 ambao watahudhuri mkutano huo ambao ni wa kikatiba.

Alisema lich ya wajumbe wamkutano huo ambao ni wanachama wa CWT pia kuna wageni waharikwa ambao wataambatana na raisi ambao ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu,makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na mawaziri.

“Nchi mbalimbali zimeaalikwa kuwakilisha nchi zao kama vyama rafiki vya walimu ambazo ni Denmark,Ireland,Canada,Afrika ya Kusini,Ghana,Kenya,Uganda,Rwanda, Burundi na Majirani zetu Zanzibar” alisema Njamasi.

“Naomba kuwahamasisha walimu wote ambao hawatapata fursa ya kufika katika mkutano wahamasike zaidi katika kufuatilia mkutano huo kwani utarushwa mbashara(live) katika vyombo mbalimbali vya habari ili watanzania wote hususani waweze kujua nini kinazungumzwa na mkuu wan chi katika mkutano huo” amesema Mwenyekiti CWT.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washiriki mbio za NBC Dodoma Marathon kutumia treni ya SGR kwenda Dodoma

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari Mchanganyiko

Upandaji miti uzingatie kuondoa umaskini kwa wananchi

Spread the loveKATIBU Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk. Musa Ally Musa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

error: Content is protected !!