Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM: Sikuwa na uhakika kama nitafanikiwa kuhamia Dodoma
Habari za Siasa

JPM: Sikuwa na uhakika kama nitafanikiwa kuhamia Dodoma

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amesema, kwa sasa Serikali yote ipo Dodoma ambapo ni mjii mkuu wa nchi kutokana na ofisi na wizara zote za serikali kuwepo jijini humo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam  … (endelea).

Hayo ameyasema leo Jumamosi tarehe 30 Mei, 2020 wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Ikulu eneo la Chamwino nje kidogo ya Jiji Dodoma.

Hafla hiyo imehudhuliwa na Mama Maria Nyerere kwa niaba ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na marais wastaafu, Ali Hassani Mwinyi, Benjamini Mkapa na Jakaya Kikwete ambao wote walishiriki kuweka jiwe la msingi.

Katika sherehe hiyo, Rais Magufuli amesema wakati wa kampeni 2015 aliahidi ndani ya miaka mitano ya utawala wake, serikali yote itakuwa imehamia Dodoma kama ilivyokuwa ndoto ya Mwalimu Nyerere.

“Niliahidi kuwa ndani ya miaka miatano Serikali yote itahamia Dodoma, lakini sikuwa na uhakika kama nitafanikisha, lakini namshukuru Mungu imewezekana, watumishi na wizara zote zimehamia Dodoma,” asema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema, pamoja na kuhamia Dodoma, wameshaboresha miundombinu kwa kujenga barabara yenye kilomita 51 kwenye mji wa Serikali pamoja na kupanua uwanja wa ndege, kujenga stendi kuu ya mabasi na kuboresha huduma ya afya kwa kuboresha Hospitali ya Benjamini Mkapa.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amewashukuru maraisi wastaafu kwa kukubali kwao kuwepo kwenye hafla hiyo kwa kuwa hakustaili kazi hii kuifanya peke yake.

 

“Sikustaili kufanya hii kazi peke yangu, ndio maana nikawaomba hawa marais wastaafu tuje kushirikiana pamoja kuweka hili jiwe na msingi na jiwe hili litawekwa na mimi, Mzee Kikwete, Mzee Mkapa, Mzee Mwinyi na mama Maria.”

“Nimefurahi sana kuwaona maraisi kwenye hafla hii, kwasababu maraisi hawa wote waliwahi kuishi kwenye Ikulu ya Dar es Salaam na kuifanya inavyo onekana hivi sasa,” amesema.

“Mzee Mkapa alifanya ukarabati mkubwa wa Ikulu na Mzee Kikwete alijenga ukumbi mkubwa wa kufanya mikutano, ndio sababu nimefarijika kuwaona maraisi wastaafu kwenye hafla hii,” amesema Rais Magufuli.

Ikulu hiyo ambayo ina eneo la kilomita za mraba 8470 ni kubwa zaidi ya Ikulu ya Dar es Salaam yenye hekali 41.8 ambayo inajengwa na vijana 2400 wa jeshi la kujenga Taifa JKT ambao amewahidi kuwalipa baada ya ujenzi kumalizika.

Akiwazungumzia vijana wa JKT wanaojenga Ikulu huyo, alianza kwa kuuliza wako wangapi, akajibiwa wako 2400, kisha vijana hao wakashangilia ambapo Rais Magufuli akawataka kuendelea kufanya kazi huku akiwaonya viongozi wao kutokuongeza idadi hiyo pindi watakapomaliza ujenzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!