April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

JPM: Pinda ana moyo wa pekee

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli amemsifu Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu kwamba ni miongoni mwa watu wema na wanamsaidia kuongoza nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kiongozi huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo tarehe 9 Oktoba 2019, wakati akizundua Barabara ya Kanazi – Kizi – Kibaoni yenye urefu wa kilomita 76.6.

Akizungumza na wananchi kweneye mkutano wake Rais Magufuli amesema, Pinda ni mtu mwema “Huyu ni mtu mwema sana na ndio maana nimemchagua kuwa mjumbe wa kamati kuu.”

Amesema, waziri mkuu huyo mstaafu amekuwa akimsaidia katika katika amsuala yale ya kiutawala “…nanisaidia kuongoza nchi, chama katika mambo mbalimbali kwa sababu ni mtu mmoja mstaarabu sana.

“Mzee Pinda ananisaidia sana katika kazi, yule baba ana moyo wa kipekee. Ni mtu mwema sana.”

Rais Magufuli anaendelea na ziara yake mkoani humo ikiwa ni pamoja na kufungua miradi ya maendeleo.

error: Content is protected !!