Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM: Nimewasamehe Makamba, Ngeleja
Habari za Siasa

JPM: Nimewasamehe Makamba, Ngeleja

Spread the love

RAIS John Magufuli amewasamehe January Makamba, aliyekuwa Waziri wa Mazingira na Muungano na Willium Ngeleja, Mbunge wa Sengerema baada ya kumwomba radhi. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Amesema, Makamba na Ngeleja walimwomba radhi baada ya sauti za mazungumzo yao kuhusu masuala mbalimbali kuvuja mitandaoni.

Akitangaza  msamaha huo leo tarehe 4 Septemba 2019 jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema amewasamehe wabunge hao baada ya kuwa waungwana kwa kujirudi na kumuomba msamaha.

“Saa nyingine kusamehe huwa kuna uma lakini saa nyingine inabidi usamehe, mi nakumbuka hivi karibuni kuna watu fulani walinitukana tuikana wee na nika ‘proove’  kwamba zile sauti ni zao kwa asilimia 100.

“… nikawa nakaa nafikiria, sema hawa wakipelekwa kwenye kamati ya siasa adhabu itakuwa kubwa, nikasema ngoja ninyamaze,”  amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema, angeweza kuwafikisha katika Kamati ya Siasa kwa kuwa alithibitisha kwamba wanahusika katika sauti hizo, lakini aliamua kuwacha kwa kuwa wangepata adhabu kubwa.

“Lakini wakajitokeza wawili wakaniomba msamaha, nikawa najiuliza mimi kila siku huwa naomba msamaha kwa Mungu na ile sala ya kuomba utusamehe makosa yetu kama tunavyowasemehe wengine, nikaona hawa waliokuja kuniomba msahama na kutoa kweli kutoka kwenye dhamira yao nisipowasamehe, nitabaki na maumivu makubwa katika moyo wangu,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;

“…nikaamua niwasamehe ambao ni mheshimiwa January Makamba pamoja na William Ngeleja, waliomba msamaha wakanigusa, nikasema hawa ni viajana na niliwasamehe nikasahau.”

Kusambaa kwa sauti zinatajwa kuwa za January na Ngeleja, liliibuka baada ya Makatibu Wakuu Wastaafu wa CCM, Mzee Yusuph Makamba na Abdulrahman Kinana tarehe 14 Julai 2019 kutoa waraka wakilalamikia kitendo cha wastaafu kuchafuliwa na baadhi ya watu pasina mamlaka husika kuchukua hatua.

Sauti ya kwanza inadaiwa kuwa ni mazungumzo ya Ngeleja na Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama wakizungumzia kuhusu waraka wa wastaafu hao wakikemea kusemwa vibaya na baadhi ya watu huku mamlaka husika zikikaa kimya.

Sauti ya pili iliyovuja inadaiwa kuwa ni ya Nape, January na Mzee Makamba wakizungumzia waraka huo.

 Baada ya kuvuja kwa sauti hizo, waliibuka watu wengi wakiwemo makada wa CCM, wakitaka chama hicho na serikali kuwachukulia hatua wahusika kwa madai kwamba wanamtuka Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!