Saturday , 9 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa JPM: Mungu kajibu maombi 
Habari za Siasa

JPM: Mungu kajibu maombi 

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS John Magufuli amesema, Mungu amejibu maombi ya Watanzania kuepusha ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virisi vya corona (COVID-19) nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea). 

Akihudhuria ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata Dodoma leo tarehe 7 Julai 2020, Rais Magufuli amesema Mungu amesikia na kupokea sala za Watanzania kuhusu kuepusha janga la corona.

“Mungu amejibu maombi ya Watanzania ambao wamesali, wamefanya toba na kufunga, na matokeo yake maambukizi ya corona yamepungua na wananchi wanaendelea na maisha yao huku wakichapa kazi, tofauti na ilivyodhaniwa kuwa corona ingesababisha madhara makubwa,” amesema Rais Magufuli.

Pia amewashukuru viongozi wa dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba Mungu aepushe janga hilo.

Kwenye kanisa hilo, Rais Magufuli ameendesha harambee ya kuchangia upanuzi wa kanisa hilo na kufanikiwa kuchangisha zaidi ya Mil 17, katika fedha hizo, yeye ametoa kiasi cha Sh. 10 milioni na mifuko 76 ya saruji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!