Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa JPM: Msipuuze wapinzani, wamebadilika
Habari za Siasa

JPM: Msipuuze wapinzani, wamebadilika

Spread the love

RAIS John Magufuli amewataka viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutobweteka kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na viongozi wa chama hicho wa mikoa na wilaya leo tarehe 24 Januari 2020, jijini Dar es Salaam Rais Magufuli amewasihi kutopuuza nguvu ya vyama vya upinzani, kwa kuwa wamebadilika.

Rais Magufuli amesema, washindani wa CCM wa leo sio wa miaka ya nyuma, kwani wamebadilika na wanabuni mikakati mingi, inayojulikana na isiyojulikana, katika kuhakikisha wanapata ushindi kwenye uchaguzi huo.

“CCM ya leo sio ya miaka ya nyuma lakini lazima tutambue pia, washindani wetu wa leo sio wa miaka ya nyuma, nao wamebadilika. Wanabuni mikakati mingi, mikakati yao mingine ya hadharani lakini mingine ya siri, tusibweteke,” amesisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, amewataka viongozi na wanachama wa chama hicho, kujiandaa vyema katika kushiriki uchaguzi huo.

“Lazima kama chama tujitathimini tuwe na uhakika wa maandalizi halisi katika uchaguzi, ni lazima tufanye hivyo kwa sababu pamekuwa na mabadiliko mengi. Na chama chetu kimebadilika, kwa hiyo ni vyema tukajidhatiti na kujiweka katika hali ya ushindi,” ameeleza Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!